Skip to main content

Posts

Showing posts from July, 2017
TIMU Mpya katika Ligi Kuu ya Tanzania  Lipuli FC  inayonolewa na   Kocha Selemani Matola katika kutaka kujiimarisha kwa ajili ya msimu mpya wa 2017-18,  imesajili kwa  wachezaji wawili wa zamani wa wa Yanga mshambuliaji Malimi Busungu na kiungo mshambuliaji Omega Seme kwa mkataba wa mwaka mmoja kila mmoja. Lipuli yenye maskani Iringa msimu ujao itatumiaSamora, katika kujipima nguvu hivi karibuni na ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Azam Fc na kufungwa mabao 4-0 kabla ya kuzinduka na kuifunga Singida United  bao 1-0..

Mastaa Uganda wamkumbuka Micho

Wachezaji wa Uganda wameanza kumkumbuka Kocha wao kutoka Serbia   Milutin 'Micho' Sredojevic  ambaye mwishoni mwa wiki alijiuzulu kuinoa timu hiyo kufuatia kutolipwa malimbikizo ya mshahara wake. Mosses Besena ameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Uganda (Fufa) kukaimu nafasi yake. Mchezaji Farouk Miya ambaye ametumia mtandao wa Twitter  kuonesha masikitiko yake kuhusu kuondoka kwa  Micho kutokana na mchanngo wake kwake na nchi, pia amemtakia kila la kheri aendako.

Karibuni Spotifleva

Na Deodatus Myonga KARIBUNI wadau wa michezo katika Blogu ya Spotifleva kwa ajili ya kupata habari mbalimbali za michezo na burudani kitaifa na  kimataifa. Ni ukweli usiopingika kukua kwa tekinolojia habari na mawasiliano kumefanya ulimwengu mzima kuungana, kwa kupitia blogu hii mashabiki na wadau mtapata habari mbalimbali za michezo na burudani. Ninawaomba mashabiki na wadau wa michezo na burudani kuiunga mkono Spotifleva kwa kuipitia na kutoa dondoo za habari ili kuandikwa na kuwafikia watu wengi zaidi kwa muda mfupi. Lengo la blogu hii ni kuwa jukwaa au daraja la kupitishia matukio mbalimbali ya michezo na burudani yanayotokea nchini na pia kimataifa kwa kutumia waandishi wa nchini na vyanzo mbalimbali vya habari kama mtandao, televisheni na redio. Spotifleva itatoa habari nzuri zenye radha za michezo na burudani zitakazofanya msomaji kuelimika na kuburudika kwa wakati mmoja. Ninawakaribisha mashabiki na wadau wa michezo kutoa sapoti kwa kupitia blogu hii mara ...

Ndondo yamrejesha Chuji Ligi Kuu

MASHINDANO ndondo yanayoendelea Dar es Salaam yamesaidia kumrejesha kiungo mkongwe   Athumani Iddi ‘Chuji’  katika  Ligi Kuu Bara, akijiunga na Ndanda FC ya Mtwara. Chuji amesaini mwaka mmoja Ndanda ilinusurika kushuka Ligi Kuu  Bara. Chuzi aliyewahi kuicheze Yanga na Simba, katika michuano ya Ndondo aliichezea timu ya Faru Jeuri, katika Ligi Kuu timu yake ya mwisho kuichezea ilikuwa ni  Mwadui FC ya Shinyanga a.

Raphael Daud aanza kujifua Yanga

BAADA ya kukamilisha dili kwa kusaini mkataba wa kuitumia Klabu ya Yanga kwa miaka miwili akitokea Mbeya City , kiungo   Raphael Daud  leo amejiunga na kambi ya timu hiyo iliyopo Morogoro. Daud amesainiwa kama mrithi wa aliyekuwa kiungo wa timu hiyo, Haruna Niyonzima ambaye ameachana na klabu hiyo na anadaiwa kusainiwa na watani wao wa jadi Simba ambao wameweka kambi Afrika Kusini. Mchezaji mwingine aliyetua hivi karibuni kabisa katika kambi ya Yanga  kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya ni Mzimbabwe Donald Ngoma. Yanga ambao ni Mabingwa watetezi watacheza mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba ambao ni Mabingwa wa Kombe la Shirikisho Agosti 23, mwaka huu kwenye uwanja wa Uhuru.

Manula aongeza utamu Simba Sauzi

KAMBI ya timu ya Simba  iliyopo nchini Afrika Kusini katika mji wa  Eden Vale, Johannesburg itachanganya zaidi kutokana na mlinda mlango Aishi Manula kuungana na wachezaji wenzie baada ya uongozi Msimbazi kumalizana na klabu ya Azam aliyokuwa akiichezea, ambayo amebakiza siku chache za kukamilisha mkataba wake. Kwa mujibu wa taarifa ya klabu hiyo iliyotolewa leo. Manula atatua bondeni kesho na kuanza kujifua na wenzie kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu 2017-18 Kombe la Shirikisho na mashindano mengine. Manula anajiunga na Simba kwa mkataba wa miaka miwili baada ya kuichezea Azam kwa zaidi ya misimu mitano akitokea katika akademi ya klabu hiyo. Hapa ni taarifa rasmi ya Simba iliyotolewa na Ofisa Habari wake, Haji Manara. SIMBA SPORTS CLUB DAR ES SALAAM 31-7-2017                       TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI __________________ Golikipa wa kimataifa wa Tanzania Aishi Salum Ma...

Wenger awakomalia Sanchez, Ozil

LONDON, Uingereza KOCHA mhenga Arsene Wenger wa Arsenal ni jeuri, hivyo ndivyo unavyoweza kusema. Babu huyo aliyeinoa Arsenal kwa miaka 21, anasema yuko tayari kuwaachia wachezaji wake kama Alexis Sanchez na Mesut Ozil  kuondoka bila ya kulipwa chochote baada ya kumaliza mikataba yao, hayuko tayari kuingia mikataba mipya kwa sharti la kuongezwa mishahara mikubwa isiyolingana na uchezaji. Kama wachezaji watatu wangeuzwa, Arsenal ingeweza kuingiza  kiasi cha pauni milioni 125 (zaidi ya sh. bilioni 366) Mfaransa huyo ambaye timu yake ilitwaa ubingwa wa Kombe la Emirates Jumapili,  alisema hawezi kuwauza wachezaji wake waliobakiza muda mfupi na wanaotaka kuondoka kwa sababu ya  kutaka kupiga pesa tu. Sanchez, Ozil, Alex Oxlade-Chamberlain, Santi Cazorla na Jack Wilshere ni miongoni mwa wachezaji ambao wamebakiza mwaka mmoja. Wenger alisema msimamo wake ni kutaka kuiona wachezaji wakicheza vizuri kujituma kuonesha thamani yao na kupata mikataba mipya...

Cristiano Ronaldo aburutwa mahakamani

MADRID, Hispania MWANASOKA nyota Cristiano Ronaldo leo ametinga katika mahakama nchini Hispania ambako anakabiliwa na mashitaka ya kukwepa mamilioni ya kodi . Waendesha mashtaka wanamtuhumu Ronaldo ambaye ni manamichezo mwenye mapato makubwa zaidi duniani kukwepa kodi ya takribani dola milioni 17.3 (zaidi ya sh, bilioni 38.7). Alitarajiwa kusema chochote baada ya kusomewa mashitaka lakini haikuwa hivyo. Nyota huyo wa Real Madrid mwenye umri wa miaka 32, awali alikanusha tuhuma hizo kwa kusema kuwa yeye ni mtu safi. Ronaldo ni mwanasoka wa mwisho katika msururu wa wanasoka walioshitakiwa na mamlaka ya kodi ya Hispania. Nyota wa Argentina,  Lionel Messi, anayeichezea Barcelona, alihukumiwa kifungo cha miezi 21 baada ya kukutwa na hatia ya kukwepa kodi mwaka jana. Mwanzoni mwa mwezi huu, mahakama ilisema anaweza kulipa  euro 252,000 (zaidi ya sh. milioni 661.6) ili asifungwe. Ronaldo alikaa mahakamani kwa muda wa saa moja na nusu, alitoa ushahidi kwa majaji...

Kuwaona Mayweather, McGregor laki 290

Kuwaona Mayweather, McGregor laki 290 NEW YORK, Marekani EDDIE Hearn amesema bondia Floyd Mayweather anataka mashabiki wa Uingereza kulipa pauni 100 (zaidi ya sh. 290,000) kwa kila mtu ili kuona katika televisheni pambano lake dhidi ya Conor McGregor, lakini kituo cha Sky kinataka iwe pauni 19 (zaidi ya sh. 55,000). Huku zikiwa zimesalia wiki nne, mashabiki bado hawajatangaziwa rasmi kuhusu ni kiasi gani watalipia ili kuona moja kwa moja pambano hilo kwenye runinga na ni kituo gani kitarusha. Eddie Hearn ambaye ni kocha wa masumbwi, amesema anahisi Mayweather atachaji kiasi hicho cha fedha kwa pambano lao litakalofanyika Agosti 26, mwaka huu mjini Las Vegas. Wakati wa pambano kati ya Mayweather  dhidi ya Manny Pacquiao mwaka 2015, kiasi cha juu cha kuona pambano hilo ilikuwa ni dola 89.99 (zaidi ya sh.200,000  na  dola 99.99 (zaidi ya sh 220,000. Katika mahojiano kati ya Eddie Hearn na GQ alisema Mayweather anapenda kiasi cha kuonesha pambano hilo kat...

Ben Foster ashiriki mbio za baiskeli

LONDON, Uingereza MLINDA mlango Benny Foster ameonesha kuwa fiti na tayari kwa kushiriki msimu mpya wa Ligi Kuu England kwa kushiriki mbio za baiskeli umbali wa maili 100 katika mji wa London. Foster mwenye umri wa miaka 34, Jumapili iliyopita aliungana na waendesha baiskeli zaidi ya 24,000 wakiwemo wa kulipwa na ridhaa katika mbio za RideLondon zinazofanyika kila mwaka. Mbio hizo zilizoanzishwa mwaka 2013 zilifanyika kwa sehemu kubwa magharibi mwa London kabla ya kwenda Surrey Hills. Waandaaji wa mbio hizo wamesema kuwa zilishirikisha zaidi ya watu100,000, Foster alimaliza kwa kutumu muda wa saa 5:01.34 alikuwa nyuma ya nahodha wa zamani wa wa timu ya taifa ya rugby ya Uingereza Martin Johnson, however. Mlinda mlango huyo alishiriki mbio hizo kwa ajili ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ugonjwa wa saratani ya tamu ambapo inatarajiwa kukusanywa pauni milioni 1 kwa ajili ya hospaitali ya Queen Elizabeth ya  Birmingham. Mbio nyingine zinatarajiwa kufanyika Velo Bir...

Neymar aaga Real Madrid

NEW YORK, Marekani MSHAMBULIAJI Neymar Santos, ameutia nguvu uvumi wa kuondoka katika timu ya Barcelona baada ya kukaa kwa dakika takribani 15 kwenye chumba cha kubadilishia jezi cha Real Madrid baada ya kuisha mchezo ambao Barcelona ilishinda mabao 3-2 mjini Miami, Marekani. Mchezaji huyo wa Brazili,  amekuwa akihusishwa na kuhamia timu ya Paris Saint-Germain kwa ada ya pauni milioni 196 ambayo imo kwenye kipengele cha mkataba wake kama kuna timu inataka kuuvunja na kumchukua. Baada ya kuisha mchezo huo wa Jumamosi, alibadilishana jezi na Sergio Ramos na Casemiro na kuonekana kama vile alikuwa akiagana na rafiki zake, taarifa nchini Hispania zimesema . Nyota huyo mwenye umri wa miaka 25, pia alionekana akiwa pamoja na mshambuliaji wa zamani wa Real Madrid na  Brazil, Julio Baptista baada ya mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Hard Rock. Neymar alitoa pasi mbili za mabao katika mchezo huo wa El Clasico ambao unaweza kuwa  mwisho kwake kama atahama huku Lione...

Mahrez ahesabu saa kutua Roma

ROMA, Italia RIYAD Mahrez kesho atafanyiwa vipimo kabla ya kusaini mkataba wake wa pauni milioni 31.3 katika timu ya Roma,  habari kutoka Italia zimesema. Mchezaji huyo Bora wa Chama cha Wachezaji wa Kulipwa England (PFA) 2015-16 ameiambia timu yake ya Leicester kwamba anataka kuondoka ili kuendeleza kipaji chake. Gazeti la Corriere dello Sport ambalo linajulikana kuwa karibu na timu hiyo ya Giallorossi limesema klabu zote mbili zimefikia makubaliano kuhusu ada huku Leicester maarufu kama 'Foxes’ (mbweha) ikitaka kumsaini Kelechi Iheanacho kutoka Manchester City kama mrithi wa Mahrez.  Mahrez baada ya kutua mjini Roma, leo anatarajiwa kupimwa afya kabla ya kusaini mkataba mpya kwa miamba hiyo ya Serie A. Arsenal na Tottenham ni timu nyingine zilizokuwa zikimsaka mchezaji huyo raia wa Algeria, lakini zilikwazwa na ada iliyokuwa ikitakiwa na timu yake. Roma ikiwa chini ya Mkurugenzi wa soka, Monchi imekuwa ikisaini wachezaji kujiimarisha baada ya kuondoka kwa Thom...

'Mnyama Okwi' atua Sauzi kumaliza utata.. !!

Tayari mnyama Emanuel Okwi ametua Sauzi kuungana na jeshi la Omog wekundu wa Msimbazi. Ujio wa mshambuliaji huyo toka SC kunazidi kuwatia tumbo joto wapinzani mbele ya safu ya ushambuliaji ya Simba SC kwa msimu wa 2017-18.

Neymar avua jezi ya Barcelona na kuamua kuondoka

Mshambuliaji wa klabu ya Barcelona Neymar Dos Santos leo ametawala upya vichwa vya habari baada ya kuvua jezi ya mazoezi ya Barcelona na kuondoka uwanjani. Neymar alikuwa mazoezini na katika hali ya kawaida kulitokea kutokuelewana kati yake na mchezaji mpya wa klabu hiyo Nelson Semedo ndipo Neymar alipokasirika. Neymar alionekana kutaka kumkabili Semedo lakini wakati anamfuata huku akionekana mwenye hasira ndipo Sergio Bosquet na Javier Mascherano walimzuia. Baada ya Neymar kuzuiwa kuendeleza ugomvi alivua jezi maalumu ya mazoezi (bibs) akaitupa pembeni kisha akaupiga mpira kwa hasira na kuondoka zake. Neymar amefanya tukio hilo katika kipindi hiki ambacho anahusishwa na uhamisho wa kwenda katika klabu ya PSG na huku ikitajwa kwamba hana furaha na Barcelona. Tukio hili limezidi kuongeza tetesi kwamba Neymar anaweza kuondoka Barca lakini Barca kwa upande wao pia wamechoshwa na tabia za Neymar haswa starehe zake.

BAADA YA ZILE "NDUNDI", HATIMAYE NEYMAR AREJEA TENA MAZOEZINI

Baada ya kuzichapa na beki mpya wa Barcelona,  Nelson Semedo , mshambuliaji Mbrazil, Neymar amerejea mazoezini. Barcelona bado iko Miami nchini Marekani na Neymar alitoka mazoezini kwa hasira baada ya ugomvi huo jana. Baadaye ikaelezwa hatarejea Hispania na Barcelona na yuko katika mpango wake wa kutaka kuondoka kujiunga na PSG ambayo inamtaka kwa udi na uvumba. Hata hivyo, leo amerejea mazoezini lakini akionekana ni mtu asiye na furaha.

TSHISHIMBI AREJEA KWAO BILA YA KUSAINI, TIMU YAKE YASUBIRIWA KUMALIZA MAMBO

Kiungo mkabaji wa Mbabane Swallows ya Swaziland, Papy Kabamba Tshishimbi, jana asubuhi aliondoka nchini kurudi kwao DR Congo, lakini ameiachia mzigo mzito Yanga iliyofikia makubaliano naye ya kumsajili. Hali hiyo, imekuja ikiwa ni siku chache tangu kiungo huyo atue nchini na kufanya mazungumzo na Yanga kwa ajili ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja waliokubaliana naye. Tshishimbi raia wa DR Congo, tayari amefanyiwa vipimo vya afya na Yanga ambavyo vimeonyesha amefuzu, hivyo yupo kamili kwa ajili ya kuichezea timu hiyo bingwa wa Ligi Kuu Bara. Taarifa za kuaminika kutoka Yanga zinaeleza, kiungo huyo amemalizana kila kitu na klabu hiyo lakini kilichobaki ni Yanga kumalizana na Mbabane kwani Tshishimbi bado ana mkataba nao wa miezi minne. Imeelezwa kuwa, kiungo atarejea nchini kujiunga na Yanga mara baada ya pande hizo mbili kumalizana katika mkataba wake wa miezi minne aliyoibakisha Mbabane. Yanga imedai makubaliano na Mbabane yatafikiwa muafaka hivi karibuni kutokan...

BAADA YA NDEMLA KWENDA SWEDEN, SHAVU LA KUCHEZA MISRI LANUKIA KWA KICHUYA

Siku chache baada ya kiungo wa Simba, Said Ndemla kwenda Sweden kufanya majaribio katika Klabu ya AFC, mshambuliaji wa timu hiyo, Shiza Kichuya anaweza akapata shavu la kucheza soka nchini Misri. Taarifa kutoka ndani ya Simba zinasema klabu moja ya Misri inamtaka Kichuya ili imsajili kwa ajili ya kuichezea timu yao na sasa wapo katika mazungumzo. Bado mazungumzo ya Simba na klabu hiyo yanaendelea na wakifikia muafaka muda wowote Kichuya ataondoka kwenda nchini humo. “Kuna timu ya Misri kupitia wakala aliyemuona Kichuya kwenye ligi na kufanya mawasiliano na sisi na tayari kuna barua wameleta wakimtaka Kichuya. “Kuna dau ambalo wamelipendekeza ili waweze kumsajili Kichuya lakini sisi hatujakubaliana nalo, hivyo tupo katika mazungumzo ya kuweza kufikia makubaliano lakini tunataka waongeze dau. “Hata hivyo, itabidi tumuachie Kichuya akacheze soka la kulipwa kwani kumzuia mchezaji kwa sasa ni sawa na bure, kwani amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake na hatutaki b...

Magazeti ya Sports na Hardnews Leo 29/07/2017:

 Simba yatimiza silaha zake 11; Okwi, Niyonzima watua Sauzi, Shaffih Dauda kakimbia 'mtiti' TFF,.. Yanga waja na bonge la usajili,Na katika Hardnews: Kigogo ACACIA anaswa kininja Airport; Spika Ndugai ageuziwa kibao,.. na Kiama kipya wala rushwa chaja..

Rick Ross ajutia kauli yake

Rapper kutoka Marekani, Rick Ross ameomba radhi kwa jamii juu ya kauli ya kutosaini wanawake kwenye lebo yake kwani angewasaini lazima angekuwa na mahusiano nao wa kimapenzi. Rick Ross ameomba radhi kupitia kipindi cha redio cha ‘The Breakfast Club’. Boss huyo wa Maybach Music Group(MMG) ameamua kurudisha mdomoni matamshi yake aliyotoa siku ya jana na kukiri kosa hilo. Ross amesisitiza kuwaelimisha jamii yake kuacha kutoa matamshi mabaya dhidi ya wanawake. Pia anafikiria kutafuta rapper wa kike wanofanya vizuri na kuwasaini. Na Laila Sued

Diamond Platnumz awashukia 'vinuka mkojo'.. niacheni na zari wangu miee !!

Diamond Platnumz ameamua kuwaumbua waliokuwa wakisema kwamba penzi lake za Zari limekufa. Pia amewajibu wanaotaka mpenzi wake abaki akiwa mnyonge baada ya kupata matatizo ya kufiwa na mama yake mzazi wiki chache zilizopita. “Kuna vichupi kunuka wanajifanya wanajua sana uchungu wa Misiba ya watu…. Mtoto wa watu katoka katika matatizo mfululizo, anatakiwa apelekwe sehem tulivu apetiwepetiwe adekezwe apate faraja!…sasa kama nyie hamna mabwana wa kuwafanyia hayo, Msijifanye ni Tamaduni na kulazimisha kila mtu awe kama nyie, eti kutwa nzima ajifungie chumbani kulia… Pambaneni na Mahusiano yenu…! Nina siku 5 za kumpetipeti… leo ndio kwanza Ya kwanza .” ameandika Diamond Instagram. Diamond amefikia hatua hiyo baada ya watu kumponda mpenzi wake Zari The Boss Lady, ambaye siku ya jana alikuwa Instalive na mkali huyo wa Eneka wakijiachi kimahaba, hali iliyofanya mitandao ya kijamii kumponda kuwa anaonyesha hana uchungu wa kufiwa na mzazi wake, kazi yake ni kujiendekeza na mapenzi. Source: Bongo5