Na Deodatus Myonga |
KARIBUNI wadau wa michezo katika Blogu ya Spotifleva kwa ajili ya kupata habari mbalimbali za michezo na burudani kitaifa na kimataifa.
Ni ukweli usiopingika kukua kwa tekinolojia habari na mawasiliano kumefanya ulimwengu mzima kuungana, kwa kupitia blogu hii mashabiki na wadau mtapata habari mbalimbali za michezo na burudani.
Ninawaomba mashabiki na wadau wa michezo na burudani kuiunga mkono Spotifleva kwa kuipitia na kutoa dondoo za habari ili kuandikwa na kuwafikia watu wengi zaidi kwa muda mfupi.
Lengo la blogu hii ni kuwa jukwaa au daraja la kupitishia matukio mbalimbali ya michezo na burudani yanayotokea nchini na pia kimataifa kwa kutumia waandishi wa nchini na vyanzo mbalimbali vya habari kama mtandao, televisheni na redio.
Spotifleva itatoa habari nzuri zenye radha za michezo na burudani zitakazofanya msomaji kuelimika na kuburudika kwa wakati mmoja.
Ninawakaribisha mashabiki na wadau wa michezo kutoa sapoti kwa kupitia blogu hii mara mara kwa mara ili kupata habari mpya na kuburudika.
Tuungane pamoja katika kuifanya Spotifleva kukua na kutoa habari kemkem za michezo na burudani.
Karibuni sana blogu ya Spotifleva kwa habari motomoto.
Comments
Post a Comment