KAMBI ya timu ya Simba iliyopo nchini Afrika Kusini katika mji wa Eden Vale, Johannesburg itachanganya zaidi kutokana na mlinda mlango Aishi Manula kuungana na wachezaji wenzie baada ya uongozi Msimbazi kumalizana na klabu ya Azam aliyokuwa akiichezea, ambayo amebakiza siku chache za kukamilisha mkataba wake.
Kwa mujibu wa taarifa ya klabu hiyo iliyotolewa leo. Manula atatua bondeni kesho na kuanza kujifua na wenzie kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu 2017-18 Kombe la Shirikisho na mashindano mengine.
Manula anajiunga na Simba kwa mkataba wa miaka miwili baada ya kuichezea Azam kwa zaidi ya misimu mitano akitokea katika akademi ya klabu hiyo.
Hapa ni taarifa rasmi ya Simba iliyotolewa na Ofisa Habari wake, Haji Manara.
SIMBA SPORTS CLUB
DAR ES SALAAM
31-7-2017
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
__________________
Golikipa wa kimataifa wa Tanzania Aishi Salum Manula kesho tarehe moja,anatarajiwa kujiunga rasimi na kambi ya klabu yetu ya Simba iliopo Eden Vale Johannesburg, nchini Afrika kusini.
Manula ambae ndio Golikipa namba moja wa nchi hii ameshamalizana kila kitu kuhusu kujiunga na klabu yetu,na ameahidi kuwapa furaha wanachama na washabiki wetu,sambamba na kuisaidia klabu kushinda mataji itakayowania msimu huu.
Wakati huo huo kesho timu ya Simba inatarajiwa kucheza mechi ya kwanza ya maandalizi ya msimu dhidi ya mabingwa wa zamani wa Afrika Orlando Pirates ya nchini Afrika kusini.
Orlando ambayo ndio klabu maarufu zaid nchini humo,imeahidi kushusha silaha zake zote muhimu ili kuwapa maandalizi ya kutosha Simba,Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kwenye dimba la Orlando liliopo jijini Johannesburg.
Mechi nyingine ya mwisho itakayochezwa na Simba nchini humo itapigwa siku ya Alhamis ya wiki hii dhidi ya mabingwa wa soka nchini humo kwa sasa Bidvest
IMETOLEWA NA...
HAJI MANARA
MKUU WA HABARI WA SIMBA
SIMBA NGUVU MOJA
Comments
Post a Comment