Mshambuliaji wa klabu ya Barcelona Neymar Dos Santos leo ametawala upya vichwa vya habari baada ya kuvua jezi ya mazoezi ya Barcelona na kuondoka uwanjani.
Neymar alikuwa mazoezini na katika hali ya kawaida kulitokea kutokuelewana kati yake na mchezaji mpya wa klabu hiyo Nelson Semedo ndipo Neymar alipokasirika.
Neymar alionekana kutaka kumkabili Semedo lakini wakati anamfuata huku akionekana mwenye hasira ndipo Sergio Bosquet na Javier Mascherano walimzuia.
Baada ya Neymar kuzuiwa kuendeleza ugomvi alivua jezi maalumu ya mazoezi (bibs) akaitupa pembeni kisha akaupiga mpira kwa hasira na kuondoka zake.
Neymar amefanya tukio hilo katika kipindi hiki ambacho anahusishwa na uhamisho wa kwenda katika klabu ya PSG na huku ikitajwa kwamba hana furaha na Barcelona.
Tukio hili limezidi kuongeza tetesi kwamba Neymar anaweza kuondoka Barca lakini Barca kwa upande wao pia wamechoshwa na tabia za Neymar haswa starehe zake.
Comments
Post a Comment