LONDON, Uingereza
KOCHA mhenga Arsene Wenger wa Arsenal ni jeuri, hivyo ndivyo unavyoweza kusema.
Babu huyo aliyeinoa Arsenal kwa miaka 21, anasema yuko tayari kuwaachia wachezaji wake kama Alexis Sanchez na Mesut Ozil kuondoka bila ya kulipwa chochote baada ya kumaliza mikataba yao, hayuko tayari kuingia mikataba mipya kwa sharti la kuongezwa mishahara mikubwa isiyolingana na uchezaji.
Kama wachezaji watatu wangeuzwa, Arsenal ingeweza kuingiza kiasi cha pauni milioni 125 (zaidi ya sh. bilioni 366)
Mfaransa huyo ambaye timu yake ilitwaa ubingwa wa Kombe la Emirates Jumapili, alisema hawezi kuwauza wachezaji wake waliobakiza muda mfupi na wanaotaka kuondoka kwa sababu ya kutaka kupiga pesa tu.
Sanchez, Ozil, Alex Oxlade-Chamberlain, Santi Cazorla na Jack Wilshere ni miongoni mwa wachezaji ambao wamebakiza mwaka mmoja.
Wenger alisema msimamo wake ni kutaka kuiona wachezaji wakicheza vizuri kujituma kuonesha thamani yao na kupata mikataba mipya na si lazima kuhama.
Alipoulizwa kama anaona vizuri kwa Ozil kuondoka na kukataa mshahara wa pauni 140,000 (zaidi ya sh. milioni 410) kwa wiki anaopata, Wenger alijibu; Ndiyo. Si suala muhimu na ninafikiri ni mfano sahihi kwa sababu kila mtu anatakiwa kucheza.
“Haiwezi kubadilika kama umebakiza miaka miwili au mmoja, unakwenda nje ya uwanja,'' alisema na kuongeza kuwa wachezaji wanatakiwa kujituma kwa kipindi chote cha mikataba yao na si kuweka masharti.
Alisema kama mchezaji ataondoka hajali. Ni kitu cha kawaida kwake na kuwashangaa waandishi ambao wanashangazwa na kitu kama hicho.
Alisema kwa baadaye waandishi wataona zaidi makocha wakikataa kuwauza wachezaji kwa kuwa ada zinakuwa kubwa sana, hakuna atataka kutoa fedha zinazotakiwa, hiyo itakuwa katika kipindi cha miaka ijayo
Taarifa zinasema mshambuliaji raia wa Chile, Sanchez atajaribu kulazimisha uhamisho wake kwenda Manchester City katika siku za karibuni.
Sanchez alitarajiwa Arsenal juzi, lakini aliweka picha yake katika Instagram na kudai ni mgonjwa.
Kuna taarifa kuwa Sanchez anataka kujiunga na Manchester City ambayo inanolewa na Pep Guardiola.
Arsenal ina wachezaji nane ambao wamebakiza mwaka mmoja kwenye mikataba yao .
Ciao....
Comments
Post a Comment