Kobe Bryant NEW YORK, Marekani TIMU ya mpira wa kikapu ya LA Laker inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Marekani (NBA) imeamua kutozitumia jezi namba 8 na 24 zilizokuwa zikitumiwa na aliyekuwa mchezaji wa timu hiyo, Kobe Bryant. Bryant mwenye umri wa miaka 39 aliyetwaa ubingwa wa NBA mara tano alitangaza, kustaafu mchezo huo Aprili 2016 baada ya kucheza kwa miaka 20 katika timu ya Lakers, akifunga pointi 60 katika mchezo wake wa mwisho. Kobe Bryant alipokuwa na umri wa miaka 21 Amestaafu akiwa na rekodi ya kuwa mfungaji pointi nyingi wa wakati wote katika timu ya Lakers na wa tatu kwa NBA akifunga pointi 33,643. "Kila wakati nilikuwa nikiota yazi yangu kutungikwa katika ukuta za chumba cha kumbukumbu cha Lakers, lakini sikuwahi kufikiria zitakuwa mbili," alisema Bryant, aliyeanza kucheza mechi yake ya kulipwa ya kwanza mwaka 1996. Jezi hizo zitastaafishwa kwa maana ya kutotumiwa na mchezaji mwingine wakati wa mapumziko katika mchezo utakaofanyika katika sher...
Comments
Post a Comment