TIMU Mpya katika Ligi Kuu ya Tanzania Lipuli FC inayonolewa na Kocha Selemani Matola katika kutaka kujiimarisha kwa ajili ya msimu mpya wa 2017-18, imesajili kwa wachezaji wawili wa zamani wa wa Yanga mshambuliaji Malimi Busungu na kiungo mshambuliaji Omega Seme kwa mkataba wa mwaka mmoja kila mmoja.
Lipuli yenye maskani Iringa msimu ujao itatumiaSamora, katika kujipima nguvu hivi karibuni na ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Azam Fc na kufungwa mabao 4-0 kabla ya kuzinduka na kuifunga Singida United bao 1-0..
Comments
Post a Comment