LONDON, Uingereza
MLINDA mlango Benny Foster ameonesha kuwa fiti na tayari kwa kushiriki msimu mpya wa Ligi Kuu England kwa kushiriki mbio za baiskeli umbali wa maili 100 katika mji wa London.
Foster mwenye umri wa miaka 34, Jumapili iliyopita aliungana na waendesha baiskeli zaidi ya 24,000 wakiwemo wa kulipwa na ridhaa katika mbio za RideLondon zinazofanyika kila mwaka.
Mbio hizo zilizoanzishwa mwaka 2013 zilifanyika kwa sehemu kubwa magharibi mwa London kabla ya kwenda Surrey Hills.
Waandaaji wa mbio hizo wamesema kuwa zilishirikisha zaidi ya watu100,000, Foster alimaliza kwa kutumu muda wa saa 5:01.34 alikuwa nyuma ya nahodha wa zamani wa wa timu ya taifa ya rugby ya Uingereza Martin Johnson, however.
Mlinda mlango huyo alishiriki mbio hizo kwa ajili ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ugonjwa wa saratani ya tamu ambapo inatarajiwa kukusanywa pauni milioni 1 kwa ajili ya hospaitali ya Queen Elizabeth ya Birmingham.
Mbio nyingine zinatarajiwa kufanyika Velo Birmingham Septemba 24, Foster anashiriki mbio hizo za hisani kumuunga mko mlinda mlango wa Wolves, Carl Ikeme ambaye anapambana na ugonjwa wa saratani ya damu.
Chanzo:MailOnline
Comments
Post a Comment