Skip to main content

TSHISHIMBI AREJEA KWAO BILA YA KUSAINI, TIMU YAKE YASUBIRIWA KUMALIZA MAMBO




Kiungo mkabaji wa Mbabane Swallows ya Swaziland, Papy Kabamba Tshishimbi, jana asubuhi aliondoka nchini kurudi kwao DR Congo, lakini ameiachia mzigo mzito Yanga iliyofikia makubaliano naye ya kumsajili.

Hali hiyo, imekuja ikiwa ni siku chache tangu kiungo huyo atue nchini na kufanya mazungumzo na Yanga kwa ajili ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja waliokubaliana naye.

Tshishimbi raia wa DR Congo, tayari amefanyiwa vipimo vya afya na Yanga ambavyo vimeonyesha amefuzu, hivyo yupo kamili kwa ajili ya kuichezea timu hiyo bingwa wa Ligi Kuu Bara.

Taarifa za kuaminika kutoka Yanga zinaeleza, kiungo huyo amemalizana kila kitu na klabu hiyo lakini kilichobaki ni Yanga kumalizana na Mbabane kwani Tshishimbi bado ana mkataba nao wa miezi minne.

Imeelezwa kuwa, kiungo atarejea nchini kujiunga na Yanga mara baada ya pande hizo mbili kumalizana katika mkataba wake wa miezi minne aliyoibakisha Mbabane.

Yanga imedai makubaliano na Mbabane yatafikiwa muafaka hivi karibuni kutokana na klabu hiyo ya Swaziland kuonyesha nia ya kumuachia Tshishimbi baada ya kumruhusu aje nchini kufanya mazungumzo na Wanajangwani.

“Kila kitu kimekamilika kwa Tshishimbi kwa maana ya dau la usajili, mshahara na mahitaji mengine anayoyataka tumekubaliana naye, alikuja kwa ajili ya kazi hiyo pekee ambayo tayari tumekamilisha.

“Alikuja kwa ruhusa ya viongozi wake na sisi baada ya mazungumzo akaondoka kwenda kwao, kazi iliyobaki ni sisi kuzungumza na Mbabane ili tumalizane nao.

“Ninaamini tutafikia makubaliano mazuri na timu hiyo ambayo imeonyesha nia ya kumuachia Tshishimbi kuja kuichezea Yanga, kwani mkataba wake umebakia miezi minne pekee, tunataka kuvunja mkataba wake,” alisema bosi mmoja wa Yanga.

Comments

Popular posts from this blog

Mbappe apewa jezi Na 29 PSG, acheka na Neymar mazoeni

Kylian Mbappe kushoto akisalimiana na  Neymar PARIS, Ufaransa MSHAMBULIAJI kinda Kylian Mbappe (18) baada ya kuhamia katika timu ya Paris Saint-Germain ya Ufaransa kwa mkopo wa msimu mmoja akitokea Monaco ametambulishwa na amefanya mazoezi kwa mara ya kwanza na mchezaji ghari zaidi duniani,Neymar Santos . Kylian Mbappe akiwa ameshika jezi namba 29 wakati wa kutambulishwa rasmi  jana.(wapili kulia) ni baba yake, Wilfried kaka yake Ethan (watatu kulia na wanafamilia wengine. Neymar anachezea pia timu ya Brazil amesajiliwa na PSG kwa  kwa pauni milioni 198 (zaidi ya sh. bilioni 578) na kuweka rekodi mpya ya usajili duniani akitokea Barcelona, ikiwa ni kiasi kilichoandikwa katika mkataba wake kinachoitaka timu inayomtaka kulipa kiasi hicho. Mbappe katika mkataba wake mpya na PSG kuna kipengele kuwa na chaguo la kuingia mkataba wa kudumu kwa ada ya pauni milioni 166 (zaidi ya sh. bilioni 484) Julai mwakani. Kama atasainiwa kwa kiasi hicho yeye na na Neymar pe...

Jezi za Kobe Bryant zastaafishwa LA Lakers

Kobe Bryant NEW YORK, Marekani TIMU ya mpira wa kikapu ya LA Laker inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Marekani (NBA) imeamua kutozitumia jezi namba 8 na 24 zilizokuwa zikitumiwa na aliyekuwa mchezaji wa timu hiyo, Kobe Bryant. Bryant mwenye umri wa miaka 39 aliyetwaa ubingwa wa NBA mara tano alitangaza, kustaafu mchezo huo Aprili 2016 baada ya kucheza kwa miaka 20 katika timu ya Lakers, akifunga pointi 60 katika mchezo wake wa mwisho. Kobe Bryant alipokuwa na umri wa miaka  21 Amestaafu akiwa na rekodi ya kuwa mfungaji pointi nyingi wa wakati wote  katika timu ya Lakers na wa tatu kwa NBA akifunga pointi 33,643. "Kila wakati nilikuwa nikiota yazi yangu kutungikwa katika ukuta za chumba cha kumbukumbu cha Lakers, lakini sikuwahi kufikiria zitakuwa mbili," alisema Bryant, aliyeanza kucheza mechi yake ya kulipwa ya kwanza mwaka 1996. Jezi hizo zitastaafishwa kwa maana ya kutotumiwa na mchezaji mwingine wakati wa mapumziko katika mchezo utakaofanyika katika sher...

Serena Williams ajifungua mtoto wa kike

Serena Williams  (kushoto) na mpenzi wake  Alexis Ohanian FLORIDA, Marekani NYOTA wa mchezo wa tenisi wa Marekani, Serena Williams amejifungua mtoto wa kike katika Kliniki mjini  Florida. Williams mwenye umri miaka 35,alilazwa katika kituo cha Afya cha St Mary's , West Palm Beach Jumatano kabla ya kujifungua. Serena mwenye rekodi ya kutwaa mataji ya mashindano makubwa ya kila mwaka 'Grand Slam' 23 alisema mwezi uliopita amepanga kurejea katika tenisi Januari mwakani kwenye michuano ya Australia. Baada ya kutolewa taarifa kuwa amejifungua salamu za pongezi zimekuwa zikimiminika kutoka kwa wanamichezo wana watu maarufu. Habari za kujifungua kwake zimetoka wakati dada yake Venus akijiandaa kwenda kucheza mechi katika mashindano ya Tenisi ya Marekani dhidi ya Maria Sakkari na kumshinda kwa seti 2-0 akipata alama 6-3, 6-4. Serena Williams akiwa na  Alexis Ohanian katika moja ya mitoko yao kabla ya kupata mtoto. "Nimefurahi sana," Venus alisem...