BAADA ya kukamilisha dili kwa kusaini mkataba wa kuitumia Klabu ya Yanga kwa miaka miwili akitokea Mbeya City , kiungo Raphael Daud leo amejiunga na kambi ya timu hiyo iliyopo Morogoro.
Daud amesainiwa kama mrithi wa aliyekuwa kiungo wa timu hiyo, Haruna Niyonzima ambaye ameachana na klabu hiyo na anadaiwa kusainiwa na watani wao wa jadi Simba ambao wameweka kambi Afrika Kusini.
Mchezaji mwingine aliyetua hivi karibuni kabisa katika kambi ya Yanga kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya ni Mzimbabwe Donald Ngoma.
Yanga ambao ni Mabingwa watetezi watacheza mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba ambao ni Mabingwa wa Kombe la Shirikisho Agosti 23, mwaka huu kwenye uwanja wa Uhuru.
Comments
Post a Comment