Emmanuel Okwi (kulia). KAMPALA, Uganda MSHAMBULIAJI wa Simba Emmanuel Okwi ameiweka Uganda katika mazingira mazuri ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2018, baada ya kufunga bao pekee dhidi ya Misri kwenye mchezo uliopigwa leo mjini Kampala, Uganda. Okwi alifunga bao hilo dakika ya 51baada ya kupata pasi kutoka kwa Abdel-Shafi na kupiga shuti lililompira El-Hadary. Baada ya kushinda mchezo huo, Uganda sasa inaongoza Kundi E kwa kuwa na pointi saba, ikifuatiwa na Misri yenye pointi sita, huku sita huku Ghana ikiwa na pointi moja baada ya kucheza mechi mbili na kesho itapambana na Congo ambayo haina pointi. Uganda itarudiana na Misri Septemba 5 mwaka huu, kabla ya kucheza na Ghana Oktoba 7 na kumaliza na Congo Novemba 8, mwaka huu.