Philippe Coutinho (kushoto) |
LONDON, Uingereza
LIVERPOOL imekubali kumuuza Philippe Coutinho kwa Barcelona kwa ada ya pauni milioni 148 (zaidi ya sh. bilioni 428), kwa mujibu wa taarifa.
Winga huyo wa Brazil amekuwa akishinikiza uhamisho kuhamia Nou Camp baada ya miamba hiyo ya La Liga kuonesha nji ya kumhitaji na kutuma ofa tatu, ikitaka akazibe pengo la Neymar aliyetimkia timu ya Paris Saint Germany kwa kuvunja mkatana kwa kutoa pauni milioni 200 (zaidi ya sh. bilioni 578).
Mtandao wa Yahoo Sport umedai kuwa Coutinho mwenye umri wa miaka 25, ambaye yuko na timu yake ya Taifa ameshaambiwa kuwa wamiliki wa timu ya Liverpool, Fenway Sports Group wamerishia maombi yake ya kutaka kuondoka.
Taarifa zimesema kuwa Liverpool imeitaka Barca kutotangaza kwamba inamchukua mchezaji huyo ili iweze kumpata mbadala wake.Hata hivyo taarifa kutoka katika gezeti la Mundo Deportivo zimesema kuwa mkataba bado haujakaribi kukamilika na Barcelona inaweza kunyoosha mikono.
Imedaiwa kuwa miamba ya Anfield imekuwa ikizipotezea ofa za Barca na timu hiyo imeamua kutafuta mchezaji mwingine.
Kama mkataba utakamilika, Liverpool inaweza kutuma ofa nyingine ya kumtaka kiungo wa Monaco, Thomas Lemar baada ya ofa mbili kukataliwa.
Pia kocha Jurgen Klopp anaweza kuelekeza mawindo yake kwa mchezaji wa Arsenal star Alex Oxlade-Chamberlain .
Liverpool juzi ilikuabali kulipa pauni milioni 48 ili kuingia mkataba na kiungo wa RB Leipzig Naby Keita, ambaye atacheza kwa mkopo msimu huu katika timu hiyo kabla ya kuanza kumtumia Anfield msimu ujao.
Dirisha la usajili kwa klabu za Ulaya linafungwa kesho saa sita usiku.
Coutinho hajaichezea Liverpool katika mwezi huu, hakufanya mazoezi na wenzie kutokana na kudaiwa kuwa mgonjwa.
Hata hivyo madaktari wa timu ya taifa ya Brazil wamesema yuko fiti na kwa sasa yuko kwenye kikosi cha timu hiyo kinachojiandaa kupambana na Ecuador ukiwa ni mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2018, Brazil imeshafuzu.
Comments
Post a Comment