Idd Mkwela |
Mwandishi Wetu
BONDIA Idd Mkwela amedai amekuwa akiogopwa na mabondia wengine kutwangana naye kwa kuogopa kipigo.
Katika pambano lake la mwisho Mkwela alimtwanga Adam Ngange.
Akizungumza juzi Mkwela alisema alipewa ofa ya kupigana na mabondia wawili, Allan Kamote wa Tanga na Mfaume Mfaume lakini wote wameingia mitini.
Allan Kamote |
Mkwela anayenolewa na Sako Mwaisege 'Dungu', amesema kwa sasa yuko vizuri na bondia yeyote atakayejitokeza kupigana na naye ajiandae kupata kichapo.
''Ukimwangalia Kamote yeye ni namba 12, nimempita mbali sana, hana ujanja, kwa sasa amechoka, ngumi zimekwisha, sasa ni zamu yangu kutamba hakuna wa kuuzima moto wangu katika uzito wa light, mimi ni mtawala wa uzito huo hivyo, akitaka kupigana na mimi ajipange sana, '' alisema Mkwela.
Mfaume Mfaume |
Kocha Mwaisege akimzungumzia Mkwela alisema yuko vizuri sana na hata katika viwango vya ubora nchini Tanzania yuko namba mbili akiwa nyuma ya bingwa wa Dunia wa GBC Ibrahimu Class 'King Class Mawe.
Comments
Post a Comment