Floyd Mayweather Jr amempongeza Conor McGrego |
NEW YORK, Marekani
FLOYD Mayweather Jr amempongeza Conor McGregor akidai ni mpiganaji mzuri pamoja na kumshinda kwa TKO katika mchezo wao uliofanyika Jumapili iliyopita Las Vegas.
Mayweather mwenye umri wa miaka 40 amesema Conor McGregor ambaye ni bingwa wa dunia wa mchezo wa ngumi mchanganyiko (UFC) ni 'mpinzani mkali' na kuongeza hakufikiria angepata upinzani mkubwa ulingoni kama ilibyokuwa katika pambano lao lililopita.
"Ni ni mshindani mgumu," Mayweather aliiambia BBC Sport na kuongeza kuwa alikuwa ni mzuri zaidi kuliko alivyokuwa akimchukulia. Lakini yeye alikuwa mzuri zaidi.
"Nilimhakikishia kila mtu kuwa pambano lisingefika mbali. Kulikuwa na hali ya kupigana ulingoni."
McGregor katika raundi za kwanza alipiga ngumi zilizompata mpinzani wake, lakini refa Robert Byrd alisimamisha pambano katika raundi ya 10 baada ya kuona McGregor akiwa amelewa na kushinda kurudisha mashambulizi.
Mayweather alisema kwua atarejea katika kustaafu kwake baada ya kuweka rekosi ya kucheza mapambano 50 na kushinda yote katika kipindi cha miaka 21.
Comments
Post a Comment