TIMU ya Liverpool imefanya kweli kwa kukamilisha uhamisho wa
Alex Oxlade-Chamberlain kutoka timu ya Arsenal kwa ada ya pauni milioni 35 (zaidi ya sh. bilioni 100).
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ameingia mkataba wa miaka mitano atakuwa akilipwa mshahara wa pauni 120,000 (zaidi ya sh. milioni 346) kwa wiki, alikataa kubakia Arsenal na kulipwa pauni 180,000 ( zaidi ya sh. milioni 519) kwa wiki.
Oxlade-Chamberlain |
Baada ya kusaini mkataba huo, Oxlade-Chamberlain aliyekatika kikosi cha timu ya Taifa ya England inayojiandaa kuchuana na Malta kesho, alisema ana hamu kubwa ya kuanza kuichezea timu ya Liverpool.
Kocha Jurgen Klopp amesema alianza kipaji cha Oxlade-Chamberlain mwaka 2014.
Liverpool imethibitisha kukamilisha uhamisho wa Oxlade-Chamberlain kwenye akaunti yao ya Twitter , kwa kuweka picha yake na ujumbe 'karibu' chini yake.
Wachezaji wengine waliosainiwa na Liverpool msimu huu ni Dominic Solanke - Chelsea (bure), Mohamed Salah - Roma, pauni milioni 34.3 na Andy Robertson - Hull, pauni milioni 10.
Comments
Post a Comment