Kuanzia kushoto ni Naby Keita (amesaini na kutolewa kwa mkopo kwa RP Leipzig , Alex Oxlade-Chamberlain, Kocha Jurgen Klopp, Thomas Lemar na Virgil van Dijk. |
LONDON, Uingereza
LIVERPOOL itatisha msimu huu kama itafanikiwa kukamilisha usajili wa wachezaji watatu leo, siku ambayo dirisha la usajili Ulaya linafungwa.
Wachezaji ambaoinapanga kuwafungia kazi ni Alex Oxlade-Chamberlain, Virgil van Dijk na Thomas Lemar lakini Philippe Coutinho anaweza kuondola Anfield.
Leo itakuwa ni siku ya pilikapilika kwa Wekundu hao, na ina matumini usajili wake utakwenda vizuri, Kocha Jurgen Klopp anataka kuwapata wachezaji hao ili kuimarisha timu yake na kuwa ya kiushindani katika Ligi Kuu England na Ligi ya Mabingwa.
Hadi sasa timu hiyo na Arsenal zimekubaliana kuhusu mkataba ambao ufafanya Oxlade-Chamberlain ambaye ni pia mchezaji wa timu ya taifa ya England kutua Anfield kwa ada ya pauni milioni 35, baada ya kukataa kujiunga na Chelsea iliyokuwa ikimhitaji.
Nyota huyo inadaiwa atakuwa akipata mshahara wa pauni 120,000 kwa wiki.
Liverpool imeshafanya makubaliano kuhusu maslahi binafsi na taarifa zinasema kuwa atapimwa afya St George's Park ambako anafanya mazoezi na timu ya England kabla ya mchezo wao wa kuwania kufuzu fainali za kombe la Dunia dhidi ya .
Pia Van Dijk anaweza kuhamia Liverpool, huku pia ikipewa nafasi ya kumnyakua kiungo wa Monaco Lemar ambaye akipatikana inaweza kumwachia Coutinho kwenda Barcelona.
Wachezaji wengine iliowasaini msimu huu ni Dominic Solanke kutoka Chelsea (bure), Mohamed Salah kutoka Roma (pauni milioni 34.3), Andy Robertson kutoka Hull (pauni milioni10) na Naby Keita ambaye imemtoa kwa mkopo kwa timu ya RP Leipzig.
Comments
Post a Comment