Paris alivyotokelezea kwenye tuzo za MTV VMA |
NEW YORK, Marekani
BINTI wa aliyekuwa mfalme wa muziki wa pop duniani, Michael Jackson 'Jacko', Paris (19) amemkumbuka baba yake ambaye kama angekuwa hai leo angetimiza umri wa miaka 59.
Michael Jackson alizaliwa Agosti 29,1958 na kufariki Juni 25, 2009 kwa matatizo ya shinikizo la damu.
Kwa kumkumbuka baba yake ameweka kwenye mtandao wa kijamii picha aliyopiga naye inayomwonesha akiwa binti mdogo akimbusu baba yake ambaye wakati huo alitimiza umri wa miaka 50.
Chini ya picha hiyo ameandika maneno; '' Nakutakia kheri siku ya kuzaliwa mpenzi wa maisha yangu, mtu pekee aliyenionesha mapenzi ya kweli yalivyo, mtu ambaye alinipatia ari ya kuishi na jinsi ya kupanga.
Paris (kulia) alipokuwa binti mdogo akimbusu baba yake Michael Jackson 'jacko' alipotimuza umri wa miaka 50, miaka tisa iliyopita. |
“ Sitajisikia kupenda tena kama nilivyokuopenda wewe. Kila wakati uko na mimi na kila wakati nitakuwa na wewe. Ingawa mimi si wewe na wewe si mimi, ninajua kwa dhati kwamba tu wamoja. Na nafsi zetu hazitabadilika. Asante kwa muujiza, milele na kila wakati.
Wakati huohuo, binti huyo wiki hii amefanya mahopjiano na Jarida la i-D na kusema kuwa hawezi kuishi maisha ya kuingiza, anapenda kuishi aisha yake halisi akiwa kama mwanamke.
Hapendi kujinyima kula ili aonekane kuwa mwembamba, anakula baga na piza za kutosha mwanzo mwisho.
Hawezi kuvaa nguo zenye vipimo za wabunifu, kama watu wengine ana makovu na alama za michubuko, alama ya kuungua kwenye miguu na mikono yake na ana 'nyama uzembe' unaotokana na mwili kuwa na mafuta.
Anasema yeye anaishi maisha anayotaka, ni mtu na si mwanasesere. Wazo kuwa wanawake wote wanatakiwa kuwa wembamba kwa dhana ya urembo, si sahihi.
Comments
Post a Comment