Pius Buswita |
Awali Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) lilitangaza kumfungia mchezaji huyo mwaka mmoja kwa kusaini mkataba wa kujiunga na klabu mbili tofauti.
Ofisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara amesema leo wanakusudia kumpeleka mahakamani Buswita kwa kusaini mkataba wa kujiunga nao, kisha akasaini mkataba mwingine na timu nyingine (Yanga).
"Tulikosa mawasiliano na mchezaji huyo mara baada ya kuingia naye mkataba jambo ambalo lilisababisha tushindwe kupeleka jina lake TFF kutokana na kushindwa kukamilisha baadhi ya taratibu," alisema.
Amesema watampeleka mahakamani kwa kuwa walimpatia fedha na hajarudisha, alisaini mktaba mbele ya mashahidi.
Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa akizungumzia suala hilo amesema anashangazwa na uamuzi uliochukuliwa na TFF kumfungia Buswita wakati Yanga imekamilisha taratibu zote, ikiwemo kuliingiza jina lake katika usajili wa mtandao na klabu yake kutoa ruhusa ya kumwachia kwao.
Mkwasa amesema anashangaa TFF hawaihoji Simba kwa kuingia kwa kuwa na mkataba unaoonesha kusainiwa Juni 2, mwaka huu kipindi ambacho mchezaji huyo alikuwa bado na mkataba na Mbao FC, kitu ambacho kinatoa nafasi kwa Mbao kuishitaki Simba.
Comments
Post a Comment