Simon Msuva (kushoto) akishangilia na Obrey Chirwa |
Mwandishi wetu
KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)imemtia hatiani mshambuliaji wa Yanga, raia wa Zambia Obrey Chirwa na Deus Kaseke katika kesi ya kumshambulia mwamuzi Ludovic Charles kwenye mchezo wa Ligi Kuu kati ya Mbao na Yanga msimu uliopita.
Hata hivyo kamati hiyo imemkuta hatia, Simon Msuva kwa kuwa katika vielelezo alionekana kumsukuma mwamuzi na kumwangusha, hivi kumpa onyo kwa kitendo hicho.
Kutokana na kuwepo shauri hilo, Chirwa alikosa mechi mbili za Yanga dhidi ya Simba, na dhidi ya Lipuli huku pia Kaseke ambaye yuko timu ya Singida United akikosa mchezo wa kwanza kati ya timu yake na Mwadui.
Msuva kwa sasa anaichezea timu ya Difaa Hassan El- Jadida ya Algeria.
Akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye ukumbi wa mikutano wa TFF, Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu, Peter Hella amesema kwamba wachezaji wote wapo huru alilaumu kusimamishwa kwa wachezaji hao kabla ya suala lao kujadiliwa na kamati husika.
Amesema baada ya kusikilishwa kwa kesi hiyo baada ya wachezaji wamekutwa hawana hatia lakini wameshatumikia adhabu ya kukosa mechi kitu ni kutotendewa haki.
Comments
Post a Comment