Evans Aveva (kushoto) na MGeoffrey Nyange 'Kaburu' |
Mwandishi wetu
VIONGOZI wa klabu ya Simba, Rais Evans Aveva na Makamu wake, Geoffrey Nyange maarufu kama Kaburu imetajwa na kuahirishwa kwa mara ya saba, huku ikipangwa kusikilizwa tena Septemba 8, mwaka huu.
Victoria Nongwa ambaye ni Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam anasikiliza kesi hiyo amesema ameiahirisha kesi hiyo ili kupisha uchunguzi wa nyaraka zilizokusanywa.
Hata hivyo, Hakimu Nongwa amewataka mawakili wa upande wa Serikali kuharakisha kufuatilia nyaraka za vielelezo zilizokusanywa ili kesi hiyo ianze kusikilizwa.
Wawili hao wanakabiliwa na mashitaka matano, yaliyofunguliwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), yakiwemo ya utakatishaji fedha, ambayo hayana dhamana na wote wapo rumande gereza la Keko tangu Juni 29, mwaka huu.
Aveva na Kaburu wanadaiwa kughushi nyaraka zinazoonesha Simba inawalipa madeni kiasi cha dola za Kimarekani 300,000 (zaidi ya shilingi milioni 672).
Inadaiwa Aveva alitoa nyaraka za uongo kwa Benki ya CRDB Tawi la Azikiwe Dar es Salaam Machi 10, 2016, la tatu ni kutakatisha fedha kinyume cha sheria, yeye na Kaburu walikula njama za kufanya uhalifu huo.
Shitaka la nne linamhusu Kaburu kutakatisha dola 300,000 na kuziweka katika Benki ya Barclays Tawi la Mikocheni mjini Dar es Salaam, na la tano ni kutakatisha fedha yeye, na kumsaidia Aveva kufanya hivyo katika benki ya Barclays baada ya kughushi nyaraka.
Comments
Post a Comment