Naomi Osaka |
NEW YORK, Marekani
BINGWA mtetezi wa mashindano ya tenisi ya Marekani kwa upande wanawake, Angelique Kerber ametolewa katika mzunguko wa kwanza wa mashindano hayo na mchezaji kinda kutoka Japan, Naomi Osaka.
Kerber ambaye ni mchezaji namba sita kwa ubora Ujerumani alizidiwa na kinda mjapan mwenye miaka 19 na jina la kinyakyusa, Naomi ambaye yuko katika namba 45 kwa ubora duniani na kushindwa kwa seti mbili kwa alama 6-3 6-1 katika Uwanja wa Arthur Ashe mjini Flushing Meadows.
Angelique Kerber |
Ilikuwa ni siku nyingine mbaya kwa Kerber mwenye umri wa miaka 29, ambaye hajatwaa taji lolote tangu alipotwaa ubingwa miezi 12 iliyopita mjini New York.
" Bado nipo mchezaji kama nilivyokuwa na mtu vile vile," alisema na kuongeza kuwa hatakata tamaa atajaribu kusahau matokeo hayo na kuangalia mbele na alimpongeza mpinzani wake kwa kucheza vizuri na umakini
Osaka, alisema ushindi huo una maana sana kwake, kwa kuwa katika mashindano yaliopita hakufanya vizuri, umesaidia kumsahaulisha.
Osaka katika mechi inayofuata atapambana na Rebecca Peterson au Denisa Allertova.
Kwa wanaume, Roger Federer ( 36), alimshinda Francis Tiafoe (19) kwa alama 4-6, 6-2, 6-1, 1-6, 6-4.
Comments
Post a Comment