Jumba la Floyd Mayweather BONDIA Floyd Mayweather amenunua jumba la kifahari kwa pauni milioni 18.9 katika eneo la Beverly Hills, California, Marekani. Jumba hilo lina vyumba sita,mabafu 10, bwawa la kuogelea na ukumbi wa sinema na vikorombwezo vingine na sehemu ya kuweka vinywaji na kunywa. Bwawa la kuogelea katika nyumba hiyo Watu wenye majumba katika mji wa Las Vegas na Miami wenye fedha. Mayweather ambaye ni bingwa wa mikanda mitano ya ubingwa, mwenye rekodi ya kucheza mapambano 50 na kushinda yote kwa sasa ametangaza kustaafu ngumi baada ya kumpiga Conor McGregor katika pambano lao la mwisho mjini Las Vegas. Mayweather alimtwanga McGregor kwa TKO raundi ya 10, anakadiriwa kupata pauni milioni 250 (zaidi ya sh. bilioni 757).
Gari alilopata ajali nalo kiungo wa Chelsea, Tiemoue Bakayoko LONDON, Uingereza MCHEZAJI wa kiungo wa Chelsea, Tiemoue Bakayoko (23) amepata ajali wakati akiendesha gari la aina ya Mercedes SUV lenya thamani ya pauni 150,000 (zaidi ya sh. milioni 454). Ajali hiyo aliipata wakati akitokea kwenye uwanja wa mazoezi wa Cobham huku kaka yake Namory akisema kuwa hapendi kuendesha gari upande wa kushoto. Katika ajali hiyo iliyotokea juzi Alhamisi, Bakayoko alipata majareha madogo. Tiemoue Bakayoko Nyota huyo alijiunga na Chelsea inanolewa na Kocha Antonio Conte katika majira ya joto yalipita kwa ada ya pauni milioni 40 akitokea timu ya Monaco amekuwa akichezeshwa kwenye kikosi cha kwanza na leo anatarajiwa kucheza mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Stoke licha ya kupata ajali hiyo. Baada ya kupata ajali hiyo iliotokea saa 10:40 ikiwa zimepita dakika tano tu tangu atoke uwanjani, katika eneo la Blundel Lane polisi waliitwa na ili kupima na kuchukua maelezo.