Kikosi cha Man United |
LONDON, Uingereza
MANCHESTER United imesema imepata mapato ya pauni milioni 581 kwa kipindi cha fedha cha 2017 huku mapato ya runinga yakiongezeka.
Katika mwaka mmoja baada ya kushinda kombe la bara Europa, na EFL klabu hiyo imekwua na mikataba 12 ya ufadhili huku mapato ya matangazo pamoja na yale yanaopatikana wakati wa mechi yakiongezeka.
Klabu hiyo ilifaidika kutoka kwa ongezeko la mapato ya runinga wakati wa kipindi cha 2016-17 ikiwa ndio mwaka wa kwanza kati ya mitatu ya makubaliano ya matangazo ya runinga.
Klabu hiyo ya Old Trafford ni ya pili katika msimamo kwa sasa.Ina alama 13 sawa na mabao na viongozi wa ligi Manchester City baada ya kucheza mechi tano la Ligi Kuu.
Juni 30 mwaka huu mapato ya matangazo yaliongezeka hadi pauni milioni 194 kutoka pauni milion 140 mwaka mmoja kabla ikiwa ni ongezeko la asilimia 38.
Msimu huu klabu hiyo imerudi katika ligi ya vilabu bingwa baada ya kushinda kombe la Yuropa dhidi ya Ajax mnamo Mei mwaka huu.
Comments
Post a Comment