Salum Mayanga |
Mwandishi wetu
KOCHA Mkuu wa timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Salum Mayanga ametangaza kikosi kipya kitakachocheza na Malawi ‘The Flame’ katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa chini ya utaratibu wa kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (Fifa), miongoni mwao wamo makipa vijana Ramadhani Kabwili wa Yanga na Peter Manyika wa Singida United.
Wiki ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (Fifa) kwa mechi za kimataifa inatarajiwa kuanza Jumatatu Oktoba 2 hadi Jumatano ya Oktoba 11, mwaka huu ambako Tanzania imekubaliana kucheza Malawi kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam Jumamosi ya Oktoba 7, 2017 katika mchezo utakaoanza saa 10.00 jioni.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo, Kocha wa yimu ya Taifa ya Tanzania, Kocha Salum Mayanga ametaja kikosi cha wachezaji 22, wakiwemo nyota watano wanacheza soka nje ya mipaka ya Tanzania akiwamo nahodha wa kikosi hicho, Mbwana Ally Samatta.
Manyanga ambaye aliteuliwa Januari 4, mwaka huu amesema kikosi hicho kinatarajiwa kuingia kambini Ijumaa Oktoba mosi, mwaka huu kwenye Hoteli ya Sea Scape iliyoko Kunduchi, Dar es Salaam.
Wachezaji walioitwa ni Aishi Manula (Simba SC), Ramadhani Kabwili (Yanga) na Peter Manyika (Singida United).
Walinzi ni Gadiel Michael (Yanga), Boniphas Maganga (Mbao FC), Abdi Banda (Baroka FC/Afrika Kusini), Kelvin Yondani (Yanga), Salim Mbonde (Simba SC), Erasto Nyoni (Simba SC) na Adeyum Ahmed (Kagera Sugar).
Viungo wa kati ni Himid Mao - Nahodha Msaidizi (Azam FC), Hamis Abdallah (Sony Sugar/Kenya), Mzamiru Yassin (Simba SC) na Raphael Daud (Yanga).
Viungo wa pembeni ni Simon Msuva (Difaa El Jadidah/Morocco), Shizza Kichuya (Simba SC), Abdul Hilal (Tusker/Kenya), Ibrahim Ajib (Yanga) na Morel Orgenes (FC Famalicao/Ureno).
Washambuliaji ni Mbwana Samatta (KRC Genk/Ubelgiji) na Mbaraka Yussuph (Azam FC).
Benchi la Ufundi la Mayanga linaundwa na yeye mwenyewe ambaye ni Kocha Mkuu, Fulgence Novatus (Kocha Msaidizi), Ame Ninje (Kocha Msaidizi), Patrick Mwangata (Kocha wa Makipa), Danny Msangi (Meneja), Dkt. Richard Yomba (Daktari wa timu), Dkt. Gilbert Kigadye (Daktari wa timu).
Comments
Post a Comment