Gari alilopata ajali nalo kiungo wa Chelsea, Tiemoue Bakayoko |
LONDON, Uingereza
MCHEZAJI wa kiungo wa Chelsea, Tiemoue Bakayoko (23) amepata ajali wakati akiendesha gari la aina ya Mercedes SUV lenya thamani ya pauni 150,000 (zaidi ya sh. milioni 454).
Ajali hiyo aliipata wakati akitokea kwenye uwanja wa mazoezi wa Cobham huku kaka yake Namory akisema kuwa hapendi kuendesha gari upande wa kushoto.
Katika ajali hiyo iliyotokea juzi Alhamisi, Bakayoko alipata majareha madogo.
Tiemoue Bakayoko |
Nyota huyo alijiunga na Chelsea inanolewa na KochaAntonio Conte katika majira ya joto yalipita kwa ada ya pauni milioni 40 akitokea timu ya Monaco amekuwa akichezeshwa kwenye kikosi cha kwanza na leo anatarajiwa kucheza mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Stoke licha ya kupata ajali hiyo.
Baada ya kupata ajali hiyo iliotokea saa 10:40 ikiwa zimepita dakika tano tu tangu atoke uwanjani, katika eneo la Blundel Lane polisi waliitwa na ili kupima na kuchukua maelezo.
Comments
Post a Comment