Jumba la Floyd Mayweather |
BONDIA Floyd Mayweather amenunua jumba la kifahari kwa pauni milioni 18.9 katika eneo la Beverly Hills, California, Marekani.
Jumba hilo lina vyumba sita,mabafu 10, bwawa la kuogelea na ukumbi wa sinema na vikorombwezo vingine na sehemu ya kuweka vinywaji na kunywa.
Bwawa la kuogelea katika nyumba hiyo |
Watu wenye majumba katika mji wa Las Vegas na Miami wenye fedha.
Mayweather ambaye ni bingwa wa mikanda mitano ya ubingwa, mwenye rekodi ya kucheza mapambano 50 na kushinda yote kwa sasa ametangaza kustaafu ngumi baada ya kumpiga Conor McGregor katika pambano lao la mwisho mjini Las Vegas.
Mayweather alimtwanga McGregor kwa TKO raundi ya 10, anakadiriwa kupata pauni milioni 250 (zaidi ya sh. bilioni 757).
Comments
Post a Comment