Diego Costa |
MSHAMBULIAJI Diego Costa amepanda ndege kutoka Brazil kwenda Hispania ikiwa ni mchakato wa kurejea katika timu ya Atletico Madrid na amesema hajisikii vibaya kutokana na jinsi alivyofanyiwa na kocha wa Chelsea, Antonio Conte.
Alipanda ndege kutoka Brazil kwenda mjini mkuu wa Madrid.
Nyota huyo baada ya kusika atapimwa afya na kumalizia taratibu za kurejea katika timu yake ya zamani.
Awali Conte alimwambia Costa kwa njia ya meseji baada ya kuisha ligi ya msimu uliopita kwamba hayumo kwenye mipango yake.
Ada ya mwanasoka huyo inakadiriwa inaweza kuwa pauni milioni 60 kwa klabu hizo mbili.
Hiki kicheko kilikuwa cha unafiki? Kocha Anthonio Conte akifurahi baada ya Costa kufunga moja ya bao msimu uliopita. |
Hata kama atajiunga na Atletico, anaweza kuanza kucheza Januari mwakani wakati ambapo timu hiyo itakuwa imemaliza adhabu yake ya kuzuiwa kutosajili kwa misimu miwili kwa kuvunja taratibu za usajili kulingana na sheria za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (Fifa).
Taarifa zinasema Blues imekubali kumuuza kwa pauni milioni 55, na nyingine milioni 5 inalipa kutokana na mafanikio yake katika timu.
Costa, mwenye 28, aliyejiunga na Chelsea kutoka Atletico mwaka 2014 kwa ada ya pauni milioni 32, atapimwa afya katika saa 48 kabla ya kusaini mkataba wa miaka minne.
Diego Costa enzi zake alipokuwa Atletico Madrid |
Alikuwa ni miongoni wachezaji waliopambana na kufanya Conte kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England katika msimu wake wa kwanza.
Costa akiwa Chelsea alifunga mabao 59 katika mechi 120 , akitwaa nayo mataji mawili ya Ligi Kuu na Kombe la Ligi moja.
Inaelezwa kuwa anaweza kupata mshahara wa pauni150,000 kwa wiki kama aliokwua akipata Chelsea baada ya kukataa kwenda China.
Costa anatarajiwa kutamb ulishwa kama mchezaji wa Atletico kabla ya Chelsea play kucheza katika uwanja wake mpya wa Wanda Metropolitano mchezo wa Ligi ya Mabingwa Jumatano ijayo.
Comments
Post a Comment