Kobe Bryant |
NEW YORK, Marekani
TIMU ya mpira wa kikapu ya LA Laker inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Marekani (NBA) imeamua kutozitumia jezi namba 8 na 24 zilizokuwa zikitumiwa na aliyekuwa mchezaji wa timu hiyo, Kobe Bryant.
Bryant mwenye umri wa miaka 39 aliyetwaa ubingwa wa NBA mara tano alitangaza, kustaafu mchezo huo Aprili 2016 baada ya kucheza kwa miaka 20 katika timu ya Lakers, akifunga pointi 60 katika mchezo wake wa mwisho.
Kobe Bryant alipokuwa na umri wa miaka 21 |
"Kila wakati nilikuwa nikiota yazi yangu kutungikwa katika ukuta za chumba cha kumbukumbu cha Lakers, lakini sikuwahi kufikiria zitakuwa mbili," alisema Bryant, aliyeanza kucheza mechi yake ya kulipwa ya kwanza mwaka 1996.
Jezi hizo zitastaafishwa kwa maana ya kutotumiwa na mchezaji mwingine wakati wa mapumziko katika mchezo utakaofanyika katika sherehe ya tukio hilo dhidi ya timu ya Golden State Warriors.
Bryant ni mchezaji wa 10kupata heshima hiyo, akwia nyuma ya Wilt Chamberlain, Elgin Baylor, Gail Goodrich, Magic Johnson, Kareem Abdul-Jabbar, Shaquille O'Neal, James Worthy, Jerry West na Jamaal Wilkes.
"Jezi za Kobe zinakaa katika nyumba sahihi sanjari na nyingine za nyota wa wakati wote," Allisema mtendaji waLakers, Jeanie Buss.
Comments
Post a Comment