Serena Williams (kushoto) na mpenzi wake Alexis Ohanian |
FLORIDA, Marekani
NYOTA wa mchezo wa tenisi wa Marekani, Serena Williams amejifungua mtoto wa kike katika Kliniki mjini Florida.
Williams mwenye umri miaka 35,alilazwa katika kituo cha Afya cha St Mary's , West Palm Beach Jumatano kabla ya kujifungua.
Serena mwenye rekodi ya kutwaa mataji ya mashindano makubwa ya kila mwaka 'Grand Slam' 23 alisema mwezi uliopita amepanga kurejea katika tenisi Januari mwakani kwenye michuano ya Australia.
Baada ya kutolewa taarifa kuwa amejifungua salamu za pongezi zimekuwa zikimiminika kutoka kwa wanamichezo wana watu maarufu.
Habari za kujifungua kwake zimetoka wakati dada yake
Venus akijiandaa kwenda kucheza mechi katika mashindano ya Tenisi ya Marekani dhidi ya Maria Sakkari na kumshinda kwa seti 2-0 akipata alama 6-3, 6-4.
Serena Williams akiwa na Alexis Ohanian katika moja ya mitoko yao kabla ya kupata mtoto. |
"Nimefurahi sana," Venus alisema na kuongeza hawezi kuelezea kuhusu furaha yake."
Wazazi wenyewe hakutoa taarifa rasmi lakini kocha wa
Serena, Patrick Mouratoglou, kupitia Twitter ameandika: "Nimefurahi sana kwa ajili yako na ninahisi hisia zako."
Serena aliutangazia ulimwengu kuhusu ujauzito wake Aprili, bila ya kutarajia kwa kuweka picha yake kwenye mtandao wa Snapchat.
Mwaka huu alitwaa ubingwa wa Australia Januari wakati akiwa na mjamzito na katika habari zilizochapishwa na jarida la Vogue mwenzi uliopita alisema kuwa alishiriki mashindano hayo kwa kutaka kutetea ubingwa
Miongoni mwa nyota waliompongeza Serena kwa mtandao ni ni mcheza tenisi, Rafa Nadal , Garbine Muguruza na mwimbaji Beyonce.
Comments
Post a Comment