Kylian Mbappe kushoto akisalimiana na Neymar |
PARIS, Ufaransa
MSHAMBULIAJI kinda Kylian Mbappe (18) baada ya kuhamia katika timu ya Paris Saint-Germain ya Ufaransa kwa mkopo wa msimu mmoja akitokea Monaco ametambulishwa na amefanya mazoezi kwa mara ya kwanza na mchezaji ghari zaidi duniani,Neymar Santos .
Kylian Mbappe akiwa ameshika jezi namba 29 wakati wa kutambulishwa rasmi jana.(wapili kulia) ni baba yake, Wilfried kaka yake Ethan (watatu kulia na wanafamilia wengine. |
Neymar anachezea pia timu ya Brazil amesajiliwa na PSG kwa kwa pauni milioni 198 (zaidi ya sh. bilioni 578) na kuweka rekodi mpya ya usajili duniani akitokea Barcelona, ikiwa ni kiasi kilichoandikwa katika mkataba wake kinachoitaka timu inayomtaka kulipa kiasi hicho.
Mbappe katika mkataba wake mpya na PSG kuna kipengele kuwa na chaguo la kuingia mkataba wa kudumu kwa ada ya pauni milioni 166 (zaidi ya sh. bilioni 484) Julai mwakani.
Kama atasainiwa kwa kiasi hicho yeye na na Neymar peke yao thamani yao itakuwa ni pauni milioni 364 ambazo ni zaidi ya sh. trilioni moja.
Wakati wa mazoezi jana, wachezaji hao walitaniana kabla ya kufanya mazoezi pamoja na wachezaji wenzao.
Kylian Mbappe (wapili kushoto) akifanya mzopezi na wachezaji wenzie wa PSG kwa mara ya kwanza tangu ahamie. |
PSG itakapocheza dhidi ya Metz in Ligue 1.
Pamoja na kufanya mazoezi kwa mara ya kwanza katika timu yake mpya kwenye Uwanja wa Centre Ooredoo, Mbappe alitambulishwa rasmi kmchezaji wa PSG katika Uwanja wa Parc des Princes .
Familia ya Mbappe pia ilifika uwanjani, alikabidhiwa jezi namba 29 atakayokuwa akiitumia kwenye timu hiyo.
Mcheza huyo alikaa pamoja na Rais wa PSG, Nasser Al-Khelaifi wakati alipokuwa akitambulishwa, na kuelezwa amekuwa akishabikia timu hiyo tangu alipokuwa ndogo.
''Imenifanya kuwa na furaha kubwa sana kujiunga na moja ya klabu kubwa duniani, ambayo ina malengo ya kuwa nzuri zaidi,' Mei nilikuwa na mawazo kwua ningepakia Monaco. Kulitokea matokio mengine yaliionifanya kubadili mawazo.
''Haikuwa muhimu kuondoka Ufaransa. Ilikuwa muhimu kurejea katika mji niliokulia,'' alisema.
Mbappe alisema si kweli kwamba kitendo cha PSG kumsaini nyota wa Brazil, Neymar kutoka Barcelona kimeshawishi kurejea Paris.
''Ni kitu cha pili kilichochangia. Ni kitu cha kusisimua kucheza naye. Lakini nimekuja kwa ajili ya mradi,'' alisema.
Na mradi huo unaanza kesho katika mchezo dhidi ya Metz kabla ya PSG kunza pampeni yake ya kucheza mashindano ya Ligi ya Mabingwa kwa kwenda kucheza na Celtic Jumanne na kisha kucheza nyumbani dhidi ya Lyon Jumapili Septemba 17, mwaka huu.
Comments
Post a Comment