Kikosi cha Simba |
WAKATI Yanga ikiwa imeondoka Dar es Salaam kwenda Unguja na kucheza mchezo mmoja dhidi ya Mlandege ya Zanzibar na kuichapa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Amaan usiku wa kuamkia leo, Simba nayo inaelekea huko leo kujiandaa kwa mchezo wao wa Ngao ya Jamii utakaopigwa Agosti 23, mwaka huu.
Yanga baada ya mchezo wao, leo imeondoka Unguja kuelekea pemba ikitakakoweka kambi yao, Simba yenyewe itaweka kambi Unguja huku ikiwa imetoka kucheza mchezo wa kirafiki jana dhidi ya Mtibwa Sugar na kuibuka na ushindi wa bao 1-0 kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam, bao lao likifungwa na Emmanuel Okwi.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kikosi chao chote kilichosajiliwa kwa ajili ya msimu huu kitakwenda Zanzibar kwa kambi ya siku 10 kabla ya kuvaana na Yanga.
Alisema kikosi hicho kikiwa huko kinatarajwia kucheza mchezo mmoja au miwili ya kirafiki.
Awali Simba iliweka kambi Johannesburg, Afrika Kusini kwa wiki mbili ambako ilicheza mechi mbili za kirafiki, ilifungwa bao 1-0 dhidi ya Orlando Pirates kabla ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya mabingwa wa nchi hiyo, Bidvest Wits, iliporejea nchini Ogosti katika Siku ya Simba ilishinda bao 1-0 dhidi ya Rayon Sports katika mchezo wa kirafiki.
Wakati huohuo, Uongozi wa Klabu ya Simba katika kutaka kurejeasha umoja, umesamehe wanachama 71 wa timu hiyo wa Tawi la Simba Maendeleo huku ukiwataka kufuta kesi yao waliyoifungua mahakamani.
Hatua ya kurejeshwa kwa wanachama haom ilikubaliwana na wanachama waliohudhuria mkutanom mkuu wa klabu hiyo uliofanyika jana Jumapili kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere, Posta jijini Dar.
Comments
Post a Comment