Ibrahim Ajibu |
Mwandishi wetu
HATIMAYE Ibrahim Ajib amefunga bao la kwanza tangu ajiunge na Yanga, wakati timu yake ikiibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mlandege ya Zanzibar kwenye Uwanja wa Amaan.
Ajibu amejiunga nja Yanga katika msimu huu akitokea kwa mahasimu wao Simba baada ya kumaliza mkataba, ambako alianza kuichezea katika timu yao ya vijana.
Yanga inayoajiandaa kwa mchezo wa Ngao ya jamii dhidi ya mahasimu weao Simba Agosti 23, mwaka huu, imewafurahisha mashabiki wake baada Jumamosi iliyopita kufungwa bao 1-0 (kwa kujifunga) dhidi ya Ruvu Shooting kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Bao jingine la Yanga katika mchezo huo lilifungwa na lilifungwa na Emmanuel Martin.
Yanga ilicheza mpira huo ikiwa njiani kuelekea Pemba ambako itaweka kambi kujianda kwa mchezo wao dhidi ya Simba .
Comments
Post a Comment