Skip to main content

Costa atoka Brazil kwenda Hispania kujiunga Atletico


Diego Costa


MSHAMBULIAJI Diego Costa amepanda ndege kutoka Brazil kwenda Hispania ikiwa ni mchakato wa kurejea katika timu ya Atletico Madrid na amesema hajisikii vibaya kutokana na jinsi alivyofanyiwa na kocha wa Chelsea, Antonio Conte.
Alipanda ndege kutoka  Brazil kwenda mjini mkuu wa Madrid.
Nyota huyo baada ya kusika atapimwa afya na kumalizia taratibu za kurejea katika timu yake ya zamani.
Awali Conte alimwambia Costa kwa njia ya meseji baada ya kuisha ligi ya msimu uliopita kwamba hayumo kwenye mipango yake.
Ada ya mwanasoka huyo inakadiriwa inaweza kuwa pauni milioni 60 kwa klabu hizo mbili. 
Hiki kicheko kilikuwa cha unafiki? Kocha Anthonio Conte akifurahi baada ya Costa kufunga moja ya bao msimu uliopita.

Hata kama atajiunga na Atletico, anaweza kuanza kucheza Januari mwakani wakati ambapo timu hiyo itakuwa imemaliza adhabu yake ya kuzuiwa kutosajili kwa misimu miwili kwa kuvunja taratibu za usajili kulingana na sheria za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (Fifa).
Taarifa zinasema Blues imekubali kumuuza kwa pauni milioni 55, na nyingine milioni 5 inalipa kutokana na mafanikio yake katika timu.
Costa, mwenye 28,  aliyejiunga na Chelsea kutoka Atletico mwaka 2014 kwa ada ya pauni milioni 32, atapimwa afya katika saa 48 kabla ya kusaini mkataba wa miaka minne.

Diego Costa enzi zake alipokuwa Atletico Madrid

Alikuwa ni miongoni wachezaji waliopambana na kufanya Conte kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England katika msimu wake wa kwanza.

Costa akiwa Chelsea alifunga mabao 59 katika mechi 120 , akitwaa nayo mataji mawili ya Ligi Kuu na Kombe la Ligi moja.
Inaelezwa kuwa anaweza kupata mshahara wa pauni150,000 kwa wiki kama aliokwua akipata Chelsea baada ya kukataa kwenda China.
Costa anatarajiwa  kutamb ulishwa kama mchezaji wa Atletico kabla ya Chelsea play kucheza katika uwanja wake mpya wa Wanda Metropolitano mchezo wa Ligi ya Mabingwa Jumatano ijayo.

Comments

Popular posts from this blog

Mbappe apewa jezi Na 29 PSG, acheka na Neymar mazoeni

Kylian Mbappe kushoto akisalimiana na  Neymar PARIS, Ufaransa MSHAMBULIAJI kinda Kylian Mbappe (18) baada ya kuhamia katika timu ya Paris Saint-Germain ya Ufaransa kwa mkopo wa msimu mmoja akitokea Monaco ametambulishwa na amefanya mazoezi kwa mara ya kwanza na mchezaji ghari zaidi duniani,Neymar Santos . Kylian Mbappe akiwa ameshika jezi namba 29 wakati wa kutambulishwa rasmi  jana.(wapili kulia) ni baba yake, Wilfried kaka yake Ethan (watatu kulia na wanafamilia wengine. Neymar anachezea pia timu ya Brazil amesajiliwa na PSG kwa  kwa pauni milioni 198 (zaidi ya sh. bilioni 578) na kuweka rekodi mpya ya usajili duniani akitokea Barcelona, ikiwa ni kiasi kilichoandikwa katika mkataba wake kinachoitaka timu inayomtaka kulipa kiasi hicho. Mbappe katika mkataba wake mpya na PSG kuna kipengele kuwa na chaguo la kuingia mkataba wa kudumu kwa ada ya pauni milioni 166 (zaidi ya sh. bilioni 484) Julai mwakani. Kama atasainiwa kwa kiasi hicho yeye na na Neymar pe...

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...