Skip to main content

Mbappe apewa jezi Na 29 PSG, acheka na Neymar mazoeni


Kylian Mbappe kushoto akisalimiana na  Neymar


PARIS, Ufaransa
MSHAMBULIAJI kinda Kylian Mbappe (18) baada ya kuhamia katika timu ya Paris Saint-Germain ya Ufaransa kwa mkopo wa msimu mmoja akitokea Monaco ametambulishwa na amefanya mazoezi kwa mara ya kwanza na mchezaji ghari zaidi duniani,Neymar Santos .

Kylian Mbappe akiwa ameshika jezi namba 29 wakati wa kutambulishwa rasmi  jana.(wapili kulia) ni baba yake, Wilfried kaka yake Ethan (watatu kulia na wanafamilia wengine.

Neymar anachezea pia timu ya Brazil amesajiliwa na PSG kwa  kwa pauni milioni 198 (zaidi ya sh. bilioni 578) na kuweka rekodi mpya ya usajili duniani akitokea Barcelona, ikiwa ni kiasi kilichoandikwa katika mkataba wake kinachoitaka timu inayomtaka kulipa kiasi hicho.
Mbappe katika mkataba wake mpya na PSG kuna kipengele kuwa na chaguo la kuingia mkataba wa kudumu kwa ada ya pauni milioni 166 (zaidi ya sh. bilioni 484) Julai mwakani.
Kama atasainiwa kwa kiasi hicho yeye na na Neymar peke yao thamani yao itakuwa ni pauni milioni 364 ambazo ni zaidi ya sh. trilioni moja.
Wakati wa mazoezi jana, wachezaji hao walitaniana kabla ya kufanya mazoezi pamoja na wachezaji wenzao.

Kylian Mbappe (wapili kushoto) akifanya mzopezi na wachezaji wenzie wa PSG kwa mara ya kwanza tangu ahamie.
Nyota hao wanaweza kucheza kwa pamoja kwa mara ya kwanza katika ligi kesho wakati
 PSG itakapocheza dhidi ya Metz in Ligue 1.
Pamoja na kufanya mazoezi kwa mara ya kwanza katika timu yake mpya kwenye Uwanja wa Centre Ooredoo, Mbappe alitambulishwa rasmi kmchezaji wa PSG  katika Uwanja wa Parc des Princes .
Familia ya Mbappe pia ilifika uwanjani, alikabidhiwa jezi namba 29 atakayokuwa akiitumia kwenye timu hiyo.
Mcheza huyo alikaa pamoja na Rais wa PSG, Nasser Al-Khelaifi wakati alipokuwa akitambulishwa, na kuelezwa amekuwa akishabikia timu hiyo tangu alipokuwa ndogo.
''Imenifanya kuwa na furaha kubwa sana kujiunga na moja ya klabu kubwa duniani, ambayo ina malengo ya kuwa nzuri zaidi,' Mei nilikuwa na mawazo kwua ningepakia Monaco. Kulitokea matokio mengine yaliionifanya kubadili mawazo.
''Haikuwa muhimu kuondoka Ufaransa. Ilikuwa muhimu kurejea katika mji niliokulia,'' alisema.
Mbappe alisema si kweli kwamba kitendo cha PSG kumsaini nyota wa Brazil, Neymar kutoka Barcelona kimeshawishi kurejea Paris.
''Ni kitu cha pili kilichochangia. Ni kitu cha kusisimua kucheza naye. Lakini nimekuja kwa ajili ya mradi,'' alisema.
Na mradi huo unaanza  kesho katika mchezo dhidi ya Metz  kabla ya PSG kunza pampeni yake ya kucheza mashindano ya Ligi ya Mabingwa kwa kwenda kucheza na Celtic Jumanne na kisha kucheza nyumbani dhidi ya Lyon Jumapili Septemba 17, mwaka huu.

Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...