![]() |
Picha mbili tofauti zinazomwonesha Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . |
MADRID, Hispania
KOCHA wa timu ya Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia, Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo.
Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti .
Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji.
"Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.
![]() |
Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa Marco Materazzi. |
"Lakini ni sehemu ya uchezaji wangu, maisha yangu. Ni moja ya vitu ambavyo ingawa havivutii, lazima tukubali kwamba tunalazimika kuchanganua."
Awali wakati wa michuano hizo Zidane ambaye alibabwa vilivyo na Materazzi katika mchezo huo alisema alifanya tukio hilo baada ya kupandwa hasira kutokana na kutukaniwa mama na dada zake, wakati wa mchezo.
Comments
Post a Comment