Skip to main content

Afrika Kusini, Sanegal kurudiana mechi Kombe la Dunia



NYON, Uswisi
TIMU za Afrika Kusini na Senegal zitarudiana tena baada kucheza mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2018 Novemba 2016 na matokeo yake kufutwa huku hukumu ya kufungiwa maisha ya refa raia wa Ghana


 Joseph Lamptey (kushoto).
Joseph Lamptey aliyechezesha mchezo huo ikikaziwa na Mahakama ya Usuluhishi wa Migogoro ya Michezo (CAS).

Katika mchezo wa awali uliopigwa Novemba 12 mwaka jana Afrika Kusini ilishinda mabao 2-1, lakini Lamptey aliadhibiwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (Fifa) kutojihusisha na mpira wa miguu maisha yote kwa upangaji matokeo.



Adhabu ya kufungiwa kwa Lamptey imekaziwa na CAS jana Jumatano, kwa hiyo sasa Afrika Kusini na Senegal zitarudiana Novemba mwaka huu.

''Kamati ya Fifa inayoratibu michezo ya kuwania kufuzu michuano ya Kombe la Dunia imeamuru kurudiwa kwa mchezo kati ya Afrika Kusini na Senegal uliofanyika Novemba 12, 2016,'' inasomeka sehemu ya taarifa ya Fifa.

''Uamuzi huu unafuatia kuthibitishwa na Mahakama ya Usuluhisi wa Michezo (CAS) kukazia hukumu ya refa, Joseph Lamptey kufungiwa maisha kwa upangaji matokeo, uamuzi uliotolewa na Kamati ya Nidhamu ya Fifa na Kamati ya Rufaa.

'' Mechi hiyo itachezwa  ndani ya Novemba 2017 katika kalenda ya kimataifa, tarehe maalumu itathibitishwa.''


Afrika Kusini ni ya mwisho katika Kundi D ikiwa na pointi moja baada ya kufutwa kwa matokeo ya mchezo kati yake na Senegal ambalo Burkina Faso inaongoza ikiwa na pointi 6 sawa na Cape Verde iliyo katika nafasi ya pili zikitofautiana uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa, Senegal ni ya tatu ikiwa na pointi 5.

Comments

Popular posts from this blog

Mbappe apewa jezi Na 29 PSG, acheka na Neymar mazoeni

Kylian Mbappe kushoto akisalimiana na  Neymar PARIS, Ufaransa MSHAMBULIAJI kinda Kylian Mbappe (18) baada ya kuhamia katika timu ya Paris Saint-Germain ya Ufaransa kwa mkopo wa msimu mmoja akitokea Monaco ametambulishwa na amefanya mazoezi kwa mara ya kwanza na mchezaji ghari zaidi duniani,Neymar Santos . Kylian Mbappe akiwa ameshika jezi namba 29 wakati wa kutambulishwa rasmi  jana.(wapili kulia) ni baba yake, Wilfried kaka yake Ethan (watatu kulia na wanafamilia wengine. Neymar anachezea pia timu ya Brazil amesajiliwa na PSG kwa  kwa pauni milioni 198 (zaidi ya sh. bilioni 578) na kuweka rekodi mpya ya usajili duniani akitokea Barcelona, ikiwa ni kiasi kilichoandikwa katika mkataba wake kinachoitaka timu inayomtaka kulipa kiasi hicho. Mbappe katika mkataba wake mpya na PSG kuna kipengele kuwa na chaguo la kuingia mkataba wa kudumu kwa ada ya pauni milioni 166 (zaidi ya sh. bilioni 484) Julai mwakani. Kama atasainiwa kwa kiasi hicho yeye na na Neymar pe...

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...