Skip to main content

Liverpool yadaiwa kukubali kumuuza Coutinho kwa Barca

Philippe Coutinho (kushoto)

LONDON, Uingereza
LIVERPOOL imekubali kumuuza Philippe Coutinho kwa Barcelona kwa ada ya pauni milioni 148 (zaidi ya sh. bilioni 428), kwa mujibu wa taarifa.
Winga huyo wa Brazil amekuwa akishinikiza uhamisho kuhamia Nou Camp baada ya miamba hiyo ya La Liga kuonesha nji ya kumhitaji na kutuma ofa tatu, ikitaka akazibe pengo la Neymar aliyetimkia timu ya Paris Saint Germany kwa kuvunja mkatana kwa kutoa pauni milioni 200 (zaidi ya sh. bilioni 578).
Mtandao wa Yahoo Sport umedai kuwa  Coutinho mwenye umri wa miaka  25, ambaye yuko na timu yake ya Taifa ameshaambiwa kuwa wamiliki wa timu ya Liverpool, Fenway Sports Group wamerishia maombi yake ya kutaka kuondoka.
Taarifa zimesema kuwa Liverpool imeitaka Barca kutotangaza kwamba inamchukua mchezaji huyo ili iweze kumpata mbadala wake.
Hata hivyo taarifa kutoka katika gezeti la Mundo Deportivo zimesema kuwa mkataba bado haujakaribi kukamilika na Barcelona inaweza kunyoosha mikono.
Imedaiwa kuwa miamba ya Anfield imekuwa ikizipotezea ofa za Barca na timu hiyo imeamua kutafuta mchezaji mwingine.
Kama mkataba utakamilika, Liverpool inaweza kutuma ofa nyingine ya kumtaka kiungo wa Monaco, Thomas Lemar baada ya ofa mbili kukataliwa.
Pia kocha Jurgen Klopp anaweza kuelekeza mawindo yake kwa mchezaji wa Arsenal star Alex Oxlade-Chamberlain .
Liverpool juzi ilikuabali kulipa pauni milioni 48 ili kuingia mkataba na kiungo wa RB Leipzig  Naby Keita, ambaye atacheza kwa mkopo msimu huu katika timu hiyo kabla ya kuanza kumtumia Anfield msimu ujao. 
Dirisha la usajili kwa klabu za Ulaya linafungwa kesho saa sita usiku.
Coutinho hajaichezea Liverpool  katika mwezi huu, hakufanya mazoezi na wenzie kutokana na kudaiwa kuwa mgonjwa.
Hata hivyo madaktari wa timu ya taifa ya Brazil wamesema yuko fiti na kwa sasa yuko kwenye kikosi cha timu hiyo kinachojiandaa kupambana na Ecuador ukiwa ni mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2018, Brazil imeshafuzu.

Comments

Popular posts from this blog

Mbappe apewa jezi Na 29 PSG, acheka na Neymar mazoeni

Kylian Mbappe kushoto akisalimiana na  Neymar PARIS, Ufaransa MSHAMBULIAJI kinda Kylian Mbappe (18) baada ya kuhamia katika timu ya Paris Saint-Germain ya Ufaransa kwa mkopo wa msimu mmoja akitokea Monaco ametambulishwa na amefanya mazoezi kwa mara ya kwanza na mchezaji ghari zaidi duniani,Neymar Santos . Kylian Mbappe akiwa ameshika jezi namba 29 wakati wa kutambulishwa rasmi  jana.(wapili kulia) ni baba yake, Wilfried kaka yake Ethan (watatu kulia na wanafamilia wengine. Neymar anachezea pia timu ya Brazil amesajiliwa na PSG kwa  kwa pauni milioni 198 (zaidi ya sh. bilioni 578) na kuweka rekodi mpya ya usajili duniani akitokea Barcelona, ikiwa ni kiasi kilichoandikwa katika mkataba wake kinachoitaka timu inayomtaka kulipa kiasi hicho. Mbappe katika mkataba wake mpya na PSG kuna kipengele kuwa na chaguo la kuingia mkataba wa kudumu kwa ada ya pauni milioni 166 (zaidi ya sh. bilioni 484) Julai mwakani. Kama atasainiwa kwa kiasi hicho yeye na na Neymar pe...

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...