Skip to main content

Bondia Mkwela awatambia Kamote, Mfaume

Idd Mkwela

Mwandishi Wetu

BONDIA Idd Mkwela amedai amekuwa akiogopwa na mabondia wengine kutwangana naye kwa kuogopa kipigo.
Katika pambano lake la mwisho Mkwela alimtwanga Adam Ngange.
Akizungumza juzi Mkwela alisema alipewa ofa ya kupigana na mabondia wawili, Allan Kamote wa Tanga na Mfaume Mfaume lakini wote wameingia mitini.

Allan Kamote

Mkwela anayenolewa na Sako Mwaisege 'Dungu', amesema kwa sasa yuko vizuri na bondia yeyote atakayejitokeza kupigana na naye ajiandae kupata kichapo.
''Ukimwangalia Kamote yeye ni namba 12, nimempita mbali sana, hana ujanja, kwa sasa amechoka, ngumi zimekwisha, sasa ni zamu yangu kutamba hakuna wa kuuzima moto wangu katika uzito wa light, mimi ni mtawala wa uzito huo hivyo, akitaka kupigana na mimi ajipange sana, ''  alisema Mkwela.
Mfaume Mfaume

Kocha Mwaisege akimzungumzia Mkwela alisema yuko vizuri sana na hata katika viwango vya ubora nchini Tanzania  yuko namba mbili akiwa nyuma ya bingwa wa Dunia wa GBC  Ibrahimu Class 'King Class Mawe.

Comments

Popular posts from this blog

Mbappe apewa jezi Na 29 PSG, acheka na Neymar mazoeni

Kylian Mbappe kushoto akisalimiana na  Neymar PARIS, Ufaransa MSHAMBULIAJI kinda Kylian Mbappe (18) baada ya kuhamia katika timu ya Paris Saint-Germain ya Ufaransa kwa mkopo wa msimu mmoja akitokea Monaco ametambulishwa na amefanya mazoezi kwa mara ya kwanza na mchezaji ghari zaidi duniani,Neymar Santos . Kylian Mbappe akiwa ameshika jezi namba 29 wakati wa kutambulishwa rasmi  jana.(wapili kulia) ni baba yake, Wilfried kaka yake Ethan (watatu kulia na wanafamilia wengine. Neymar anachezea pia timu ya Brazil amesajiliwa na PSG kwa  kwa pauni milioni 198 (zaidi ya sh. bilioni 578) na kuweka rekodi mpya ya usajili duniani akitokea Barcelona, ikiwa ni kiasi kilichoandikwa katika mkataba wake kinachoitaka timu inayomtaka kulipa kiasi hicho. Mbappe katika mkataba wake mpya na PSG kuna kipengele kuwa na chaguo la kuingia mkataba wa kudumu kwa ada ya pauni milioni 166 (zaidi ya sh. bilioni 484) Julai mwakani. Kama atasainiwa kwa kiasi hicho yeye na na Neymar pe...

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...