Skip to main content

Neymar aaga Real Madrid








NEW YORK, Marekani

MSHAMBULIAJI Neymar Santos, ameutia nguvu uvumi wa kuondoka katika timu ya Barcelona baada ya kukaa kwa dakika takribani 15 kwenye chumba cha kubadilishia jezi cha Real Madrid baada ya kuisha mchezo ambao Barcelona ilishinda mabao 3-2 mjini Miami, Marekani.

Mchezaji huyo wa Brazili,  amekuwa akihusishwa na kuhamia timu ya Paris Saint-Germain kwa ada ya pauni milioni 196 ambayo imo kwenye kipengele cha mkataba wake kama kuna timu inataka kuuvunja na kumchukua.

Baada ya kuisha mchezo huo wa Jumamosi, alibadilishana jezi na Sergio Ramos na Casemiro na kuonekana kama vile alikuwa akiagana na rafiki zake, taarifa nchini Hispania zimesema .

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 25, pia alionekana akiwa pamoja na mshambuliaji wa zamani wa Real Madrid na  Brazil, Julio Baptista baada ya mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Hard Rock.

Neymar alitoa pasi mbili za mabao katika mchezo huo wa El Clasico ambao unaweza kuwa  mwisho kwake kama atahama huku Lionel Messi, Ivan Rakitic  na Gerard Pique wakifunga mabao kwa timu yao inayonolewa na kocha Ernesto Valverde.

Mlinzi wa Madrid, Ramos amesema kuwa kama Neymar ataondoka inaweza kuwa kitu kizuri kwa timu yake na kocha wao,  Zinedine Zidane.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo kuhusu Neymar, Ramos  alisema, ''Sijui kila mmoja yuko huru kuchagua kuhusu hatima yake ya baadaye. Ninatumaini (kama atahama) itakuwa ni tatizo dogo kwetu.''

Kocha Valverde kwa upande wake alisema baada ya mchezo kwamba anatumaini Neymar kubakia Barcelona  na waataanza naye msimu mpya wa La Liga mwezi huu.

Wakati huohuo,  habari nyingine zinasema kuwa  Neymar huenda akapimwa afya katika timu ya Paris Saint-Germain wiki hii.

Comments

Popular posts from this blog

Mbappe apewa jezi Na 29 PSG, acheka na Neymar mazoeni

Kylian Mbappe kushoto akisalimiana na  Neymar PARIS, Ufaransa MSHAMBULIAJI kinda Kylian Mbappe (18) baada ya kuhamia katika timu ya Paris Saint-Germain ya Ufaransa kwa mkopo wa msimu mmoja akitokea Monaco ametambulishwa na amefanya mazoezi kwa mara ya kwanza na mchezaji ghari zaidi duniani,Neymar Santos . Kylian Mbappe akiwa ameshika jezi namba 29 wakati wa kutambulishwa rasmi  jana.(wapili kulia) ni baba yake, Wilfried kaka yake Ethan (watatu kulia na wanafamilia wengine. Neymar anachezea pia timu ya Brazil amesajiliwa na PSG kwa  kwa pauni milioni 198 (zaidi ya sh. bilioni 578) na kuweka rekodi mpya ya usajili duniani akitokea Barcelona, ikiwa ni kiasi kilichoandikwa katika mkataba wake kinachoitaka timu inayomtaka kulipa kiasi hicho. Mbappe katika mkataba wake mpya na PSG kuna kipengele kuwa na chaguo la kuingia mkataba wa kudumu kwa ada ya pauni milioni 166 (zaidi ya sh. bilioni 484) Julai mwakani. Kama atasainiwa kwa kiasi hicho yeye na na Neymar pe...

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...