Skip to main content

Yanga, Simba sasa kupambana Okt 28



Mwandishi wetu
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa ratiba mpya ya Ligi Kuu baada ya wajumbe waliochaguliwa kufanya mapitio katika ratiba ya awali na kufanya marekebisho kama wakibaini upungufu kukamilisha kazi hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa ya iliyotolewa na Ofisa Habari wa shirikisho hilo, Alred Lucas, mabingwa watetezi Yanga watapambana na watani wao wa jadi Simba Oktoba 28, mwaka huu katika mzunguko wa nane huku mchezo wa marudiano ukipangwa katika mzunguko wa 23, Machi 14 mwakani, lakini itategemea ushiriki wao katika Mashindano ya Kimataifa ya Klabu bingwa na Shirikisho.
Tofauti na kipindi cha nyuma ambapo timu ya Azam ilikuwa ikicheza mechi zake za nyumbani dhidi ya Simba na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, safari hii itatumia uwanja wake wa Azam Complex ambao una uwezo wa kuchukua mashabiki 7,000.
Ratiba mpya, imezingatia kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (Fifa) na ile ya Shirikisho la Afrika, baada ya michezo ya Agosti 26 na 27, Ligi Kuu ya Vodacom kwa sasa itaendelea Septemba 9 na 10  mwaka huu.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Yanga, baada ya kucheza na Lipuli na kutoka nayo sare ya bao 1-1 na Lipuli, Jumamosi ijayo itacheza dhidi ya Njombe Mji, kisha kwenda kucheza na Majimaji, Songea,  kabla ya kurejea Dar es salaam  kucheza na Ndanda katika mchezo wa mzunguko wa nne Septemba 23 , mwaka huu.
Simba iliyoanza ligi kwa ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting itacheza ugenini dhidi ya Azam Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Azam Complex, kisha kucheza na Nyumbani Uwanja wa Uhuru dhidi ya mwadui katika mzunguko wa tatu kicha kwenda kucheza na Mbao FC katika mzunguko wa nne Septemba 21 na kuchuana na  Stand United katika Uwanja wa Kambarage Oktoba Mosi, mwaka huu.
Mechi za mwisho katika  ligi hiyo zitafanyika Mei 26 mwaka huu.  

Ifuatayo ni ratiba kamili ya Ligi Kuu ya Vodacom.








Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...