![]() |
| Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr |
MADRID, Hispania
MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake.
Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa haraka, lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo.
Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake.
Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti.
Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo.
Mtoto atakayemzaa atakuwa ni kwanza kwa Ronaldo mwenye umri wa miaka 32 kuzaliwa na mama anajulikana ambaye si wa kujitolea kushika ujauzito na kujifungua, lakini kutohusika na malezi.
Juni mwaka huu Ronaldo aliwapokea watoto pacha Eva Maria na Mateo na kuungana na mwanaye Cristiano Jr mwenye umri wa miaka saba.
Pamoja na kwamba amekuwa hana ukaribu na wazazi wake, Rodriguez amekuwa karibu sana na mpenzi wake Ronaldo ambaye anaishi naye na mtoto Ronaldo jr.
Pia vyombo vya habari vimesema kuwa ana uhusiano mzuri mama yake, Ronaldo Dolores Aveiro.
Georgina na Ronaldo wamekuwa pamoja tangu walipokutana mwaka jana katika anao la
VIP kwenye hafla ya Dolce & Gabbana.

Comments
Post a Comment