LONDON, Uingereza
TIMU ya West Ham imepata ushindi wake wa kwanza katika Ligi Kuu England baada ya kuichapa timu iliyopanda faraja msimu huu Huddersfield mabao 2-0.
Kipigo hicho pia kimekuwa cha kwanza kwa Huddersfield ambayo iko nafasi ya sita kwenye msimamo ikiwa na pointi saba, ambayo katika mechi zake tatu zilizotangulia, ilishinda mbili kutoka sare moja.
Matokeo hayo yameifanya, West Ham kupata pointi tatu za kwanza baada ya kupoteza mechi tatu za kwanza, iko katika nafasi ya 18 kwenye msimamo wa timu 20.
Mabao ya ushindi ya West Ham, inayonolewa na Kocha Slaven Bilic yalifungwa na Pedro Obiang dakika ya 72 ambaye alipiga shuti lililombabatiza mgongoni Mathias Jorgensen na kumpita mlinda mlango Jonas Lossl.
Javier Hernandez alipiga shuti na kugonga mwamba na kufanya West Ham kupoteza nafasi nyingine ya kufunga.
Andre Ayew aliyetokea benchi alifunga bao la pili West Ham dakika tano baadaye.
Huku zikiwa zimesalia dakika 10, mshambuliaji wa Huddersfield, Thomas Ince alipiga mpira na kugonga mwamba.
Ufuatao ni msimamo wa Ligi Kuu England baada ya kuisha mechi za mzunguko wa nne jana.

Comments
Post a Comment