![]() |
| Thomas Lemar |
LONDON, Uingereza
KIUNGO mchezeshaji Thomas Lemar aliamua kubakia Monaco badala ya kujiunga na Arsenal, amesema kocha wa timu hiyo Arsene Wenger.
Gunners ilituma ofa ya pauni milioni 92 (zaidi ya sh. bilioni 267) katika siku ya mwisho kabla ya dirisha la usajili kufungwa, ikitaka huduma ya Lemar, mchezaji ambaye ilitegemea angekuwa mrithi wa Alexis Sanchez kama angeondoka.
![]() |
| Kocha Arsene Wenger |
Sanchez alikuwa akitakiwa na Manchester City, lakini Arsenal ilijiwekea malengo ya kumpata mrithi wake kwanza ndipo imwachie.
Madai mengine ni kwamba, Lemar alikataa alikataa kujiunga na Arsenal na Wenger amejitokeza kuthibitisha Gunners isingeweza kumpata mchezaji wa kuziba pengo la Sanchez kwa wakati.
Akizungumzan na beIN SPORT, Wenger alisema:'' Mchezaji alichagua kubaki Monaco . Unatakiwa kuheshimu kitu kinachotokea katika makubaliano. Ninajua kuwa tunaishi katika wakati wa uwazi, lakini kwa kiasi fulani kumheshimu kila mtu. Hutakiwi kuzungumza sana kuhusu hilo.”


Comments
Post a Comment