Skip to main content

Wenger amlinganisha Mbappe na Pele

Kylian Mbappe

PARIS, Ufaransa
ARSENE Wenger anaamini Kylian Mbappe anaweza kuwa Pele (mchezaji wa zamani wa Brazil) ajaye katika soka baada ya kuhamia katika timu ya Paris Saint-Germain mkopo katika majira haya ya joto.
Wenger amesema haoni kama kuna ukomo wa umuhimu wa mchezaji huyo kinda.
Akizungumza na na kituo cha runinga cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot, Wenger alisema: “Mbappe anaweza kuwa  Pele ajaye.
“Hakuna ukomo wa umbali ambao anaweza kwenda.”
Alisema: “ Pia nilimhitaji, lakini dau la euro milioni 180 ni kubwa mno kwetu. Amekuwa akicheza vizuri kama mshambuliaji.

Pele

“Anafunga mabao na anatengeneza nafasi, Ni mchezaji mwenye ubora.
Mchezaji huyo wa Ufaransa, amehamia PSG katika siku ya mwisho ya dirisha la usajili kwa mkopo,  inaweza kumsaini  katika majira ya joto yajayo kwa ada ya pauni  milioni 162.
Akiwa na miaka 18 alicheza kwa kiwango cha hali ya juu kwenye timu ya Monaco msimu uliopita, aliisaidia kutwaa ubingwa wa Ufaransa na kufika nusu fainali Ligi ya Mabingwa.

Arsene Wenger

Katika msimu uliopita Mbappe  aliifungia AS Monaco mabao  26 katika mechi 44 na kuchanguliwa kuichezea timu ya taifa.

Kutokana na kuwa na kiwango kizuri wakati wa uhamisho timu nyingi za  Ulaya zilihusishwa na kumtaka ikiwemo Real Madrid na Arsenal.
Inajulikana Gunners ilituma ofa ya pauni milioni123 kwa ajili ya kumtaka Mbappe Julai mwaka huu.
Wenger pia alithibitisha kutuma ofa ya pauni milioni 91 kwa Monacco kwa ajili ya kumtaka Thomas Lemar katika siku ya mwisho ya usajili.

Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...