Skip to main content

Wenger akiri kukaribia kuondoka Arsenal

Arsene Wenger
LONDON, Uingereza
ARSENE Wenger (67) amekiri kwa mara ya kwanza kwamba alikaribia kuondoka katika kiti cha ukocha mwanzani mwa mwaka huu, na sasa lazima ajutie uamuzi wake wa kutofuata dhamira yake.
Wenger aliiambia alikiambia kituo cha televisheni cha
Telefot cha ufaransa jana kuwa alisita kusaini mkataba  mwingine Arsenal kutokana na kuwa na wasiwasi kama endelee kuwa kocha wa Gunners au la, kwa maoni hayo ina maana kuwa alikaribia kuacha kuinoa timu hiyo baada ya kuitumikia kwa zaidi ya miaka 20.
"Ndiyo, Nilisita kuongeza mkataba kwa sababu binafsi. Nimekuwa Arsenal kwa miaka 20, na ninajiuliza kama nitaendelea kuiongoza klabu.  Tulikwenda vibaya sana katika msimu."
Katika msimu uliopita Wenger  aliisaidia Arsenal kutwaa ubingwa wa saba wa Kombe la FA katika Uwanja wa Wembley Mei mwaka huu inawezekana ulichangia kuamua kuongeza mkataba mwaka mmoja.
Baada ya kuanza msimu huu vibaya, akishinda mchezo mmoja dhidi ya Leicester City mabao 4-3 kabla ya kufungwa  bao 1-0 dhidi ya Stoke  na mabao 4-0 dhidi ya Liverpool, Wenger amekuwa akijaribu kuwashawishi mashabiki kuwa na imani naye ili aendelee kuiongoza timu.
Wenger akizungumza na  beIN Sport TV Ijumaa alikanusha kwamba klabu ilikuwa ikitaka kumuuza Alexis Sanchez kwa Manchester City katika siku ya mwisho ya uhamisho.
Arsenal ilijaribu kumsaini kiungo wa Monaco, Thomas Lemar katika siku ya mwisho ya uhamisho  na kutuma ofa ya zaidi ya milioni 90 lakini ilimkosa.
Wenger kwa sasa yuko kwenye hatari ya kumkosa
 Sanchez na Mesut Ozil katika majira ya joto yajayo kwa kuwa watakuwa wamemaliza mikataba yao huku
Alex Oxlade-Chamberlain akiwa amehamia Liverpool kwa ada ya pauni milioni 35.
Mashabiki wametishia kususia mechi ya Jumamosi wakati Arsenal itakapocheza na Bournemouth katika uwanja wa Emirates ikiwa ni sehemu ya kushinikiza Wenger aondoke.
Wachezaji wa zamani wa timu hiyo Wright na Martin Keow na wanaunga mkono kocha huyo aachie ngazi.
Wamiliki wa timu wamekuwa wakimuunga mkono Wenger kwa kuwa amekuwa akiifanya timu kujiendesha kwa faida.
Kocha wa Jose Mourinho United aliwahi kukejeli kuwa kocha pekee  aliye kazini ambaye anafanya kazi bila ya kuogopa kutimliwa kwa timu kufanya vibaya ni Wenger.

Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...