Skip to main content

Wachezaji Wabrazil wakodiwa ndege kurejea Uingereza, Ufaransa


Nyota wa  Liverpool  Coutinho na Roberto Firmino, Chelsea winga Willian na wa Manchester City, Fernandinho, Gabriel Jesus na mlinda mlango Ederson wakiwa kwenye ndege ya kukodi kurejea England wakitokea Colombia usiku wa kuamkia leo.

LONDON, Uingereza
TIMU za Liverpool na Manchester City na Chelsea zimekodi ndege maalumu kuwarejesha England wachezaji wao wanaochezea timu ya Brazil, Philippe Coutinho, Fernandinho, Gabriel Jesus, Ederson, Roberto Firmino na Willian.
Nyota wa  Liverpool  ni Coutinho na Roberto Firmino, Chelsea ni winga Willian na wa Manchester City ni Fernandinho, Gabriel Jesus na mlinda mlango Ederson. 
Wachezaji hao wamechuliwa usiku wa jana kurejea Uingereza ili kucheza katika mechi za mwishoni mwa wiki za Ligi Kuu England.
Coutinho ambaye alikuwa na timu ya Brazil iliyocheza dhidi ya Colombia jana na kutoka sare ya bao 1-1 katika mechi ya michuano ya kuwania kombe la Dunia 2018 anaweza kucheza mechi yake ya kwanza katika timu ya Liverpool msimu huu wakati itakapocheza Manchester City.


Neymar (kulia) akiwa kwenye ndege ya kukodi kutoka Brazil kuelekea paridi Ufaransa akiwa an wachezaji wenzie (Lishoto kwenda kulia) Thiago Silva, Dani Alves, Filipe Luiz, Marquinhos na Jemerson

Nyota huyo alikuwa gumzo wakati wa dirisha la usajili ambapo Barcelona ilituma ofa tatu kutaka kumsaini lakini Liverpool ilikataa licha ya mwenyewe kuondoka barua kuomba aruhusiwe kuondoka. Liverpool iliweka msimamo kuwa hauzwi kwa bei yoyote.
Pia Neymar aliondoka na timu nzima ya Brazil kabla ya kupanda ndege ya kukodi kurejea Ufaransa kwa ajili ya kuendelea na michezo ya ligi.
Nyota huyo wa PSG ametupia picha kwenye akaunti yake ya Instagram inayomwonesha akiwa pamoja na wachezaji wenzie katika timu moja Thiago Silva, Dani Alves na Marquinhos,  pia  mlinzi wa Atletico Madrid, Filipe Luiz  na wa Monaco, Jemerson. 
Klabu za Ulaya  zimeshirikiana kulipa gharama za kukodi ndege ili kuwarejesha haraka wachezaji wao kwenye timu zao kwa ajili ya kuwatumia kwenye Ligi Kuu ya nchi zao na Ligi ya Mabingwa.

Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...