Kwa wa mujibu wa taarifa ya TFF iliotolewa kwa vyombo vya habari leo mchezo huo utafanyika Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, Dar es Salaam, kiingilio katika sehemu ya VIP yenye viti 1,000 kitakuwa sh. 10,000 na sh.7,000 katika sehemu ziliosalia za mzunguko zenye viti 6,000.
Uwanja huo una uwezo wa kuchukua watazamani 7,000.
TFF tiketi hizo zimeanza kuuzwa leo Jumatano ili kujiepusha na usumbufu wa aina yoyote.
Imesema mashabiki watakaokosa tiketi ni bora wasiende uwanjani wakifanya hivyo watahesabiwa kufanya vurugu.
Imesema vyombo vya usalama vitakuwa makini kudhibiti kila aina ya vurugu uwanjani hapo hasa ikizingatiwa mchezo huo utafanyika wakati jua limezama kuanzia saa 1.00 usiku.

Comments
Post a Comment