![]() |
| Polisi wakiwa na mbwa wakiwadhibiti mashabiki wa timu ya Cologne katika Uwanja wa Emirates usiku wa kuamkia leo. |
![]() |
| Mashabiki wa timu ya Cologne wakiwa mtaani kabla ya kuanza kwa mchezo dhidi ya Arsena juzi. |
PARIS, Ufaransa
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu la Ulaya (UEFA) limeziifungulia mashtaka timu za Arsenal na Cologne kutokana vurugu zilizotokea kabla ya mchezo wao wa Ligi ya Europa.
Kabla ya mchezo huo maelfu ya mashabiki wa Ujerumani walifurika kwenye uwanja wa Emirates kwa ajili ya kushuhudia mchezo wa kwanza wa timu hizo wa Ligi ya Europa.
Arsenal imefunguliwa mashtaka kuziba njia kwenye uwanja (jukwaani) huku Cologne ikiwa na mashtaka manne ya kuwasumbua mashabiki, kulipua baruti, kurusha vitu uwanjani na kufanya uharibifu.
![]() |
| Shabiki wa Cologne akimwaga moshi. |
Katika mchezo huo wa Kundi H, Arsenal ilishinda mabao 3-1, mchezo ulichelewa kuanza kwa takriban saa moja kutokana na mashabiki wengi wa timu ya Cologne waliokuwa hawana tiketi kutaka kuingia uwanjani.
Wageni hao walikuwa wametengewa tiketi 3,000,lakini kulikuwa na mashabiki takriban 20,000 waliosafiri kutoka Ujerumani na kuwasili London.
Kulikuwa na maelfu ya mashabiki wa timu hiyo waliokaa kwenye viti vya Arsenal na kusababisha usalama kuwa katika hatari.
Mashabiki watano walikamatwa katika kadhia hiyo na jioni jana ilitoa taarifa ikieleza kuwa ilijali usalama wa mashabiki katika na kusema inachunguza matukio katika mchezo huo.
Katika taarifa yake jana UEFA imesema itashughulikia kesi hiyo Septemba 21, mwaka huu.




Comments
Post a Comment