![]() |
| Mwenyekiti wa TASWA anayemaliza muda wake, Juma Pinto na Katibu wake, Amir Mhando walipokuwa wakipongeza na baada ya kutangazwa washindi katika uchaguzi uliopita. |
Mwandishi wetu
UCHAGUZI wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) utafanyika ufanyike Novemba 5, mwaka huu Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Katibu Mkuu wa Taswa, Amir Mhando, tarehe hiyo imepangwa na Kamati ya Utendaji ya chama hicho iliyokutana juzi.
Alisema uchaguzi huo utafanyika Dar es Salaam katika ukumbi utakaongazwa baadaye na tayari kamati hiyo imeaigiza sekreterieti ya TASWA kufanya maandalizi kuhusu uchaguzi huo, ikiwa ni pamoja na kulishirikisha Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kwa ajili ya usimamizi wa karibu.
Alisema watakaoshiriki uchaguzi huo ni wanachama wote wa TASWA waliopo katika leja kuanzia Juni mwaka 2007 hadi Juni mwaka 2017, wakiwemo walioingia wakati wa semina ya waandishi chipukizi iliyofanyika Dar es Salaam Agosti mwaka 2015, ili kushiriki kila mwanachama anatakiwa kulipia ada ya mwaka mmoja.
Kwa wanachama wengine wapya wanaotaka kujiunga, watafanya hivyo baada ya uongozi mpya kuingia madarakani na kupewa utaratibu kulingana na katiba ya chama inavyoeleza .
Aliongeza wanachama wote wenye sifa hizo, wanatakiwa kulipia ada kwa Mhazini Msaidizi, Zena Chande, imeanza jana hadi Septemba 30, mwaka huu.
Uchaguzi huo unafanyika baada uongozi unaomaliza muda kukaa madarakani miaka mitatu.
Viongozi hao ni Juma Pinto (Mwenyekiti), Egbert Mkoko (Makamu Mwenyekiti), Amir Mhando (Katibu Mkuu), Grace Hoka (Katibu Mkuu Msaidizi), Shija Richard (Mhazini) na Zena Chande (Mhazini Msaidizi).
Wajumbe ni Rehure Nyaulawa, Chacha Maginga, Mussa Juma, Mwani Nyangassa, Mroki Mroki, Ibrahim Bakari na Majuto Omary anayeingia kwa nafasi yake ya Mwenyekiti wa TASWA FC.

Comments
Post a Comment