![]() |
| Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo, Yusuph Singo akimkabidhi Bendera ya Taifa Nahodha wa timu ya taifa ya wanawake ya soka umri chini ya miaka 20, Dar es Dalaam jana. |
NAHODHA wa Kikosi cha timu ya Taifa ya soka ya Tanzania chini ya umri wa miaka 20 ya wanawake 'The Tanzanite' Wema Richard, amesema wanamatumini ya kufanya vizuri katika mchezo wao wa kufuzu kwa fainali za kombe la dunia 2019 nchini Ufaransa dhidi ya Nigeria.
Akizungumza wakati wa kuangwa kwa timu hiyo jana, Wema amesema wana matumini kushinda katika mchezo huo, wanawafahamu wapinzani wao kwa kuona mechi zao katika video, wanazijua mbinu zao.
''Tushawahi kuwaona wakicheza, ni timu nzuri, ni muda sasa najua watakuwa wamebadilika kwani siku zinaenda, tayari tunatahadhari ya kucheza nao tunajua tutawashinda," alisema Wema
Baada ya kukabidhiwa bendera jana, timu hiyo imeondoka kwenda Nigeria kwa ajili ya mchezo wao unaotarajwia kupigwa mwishoni mwa wiki.
Akiwaaga wachezaji wa timu hiyo, Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo, Yusuph Singo aliwataka kujituma na kuhakikisha wanashinda mechi zao ili kufuzu Kombe la Dunia kwa manufaa yao na nchi.
Kocha wa Tanzanite, Sebastian Mkoma alitamba timu hiyo inaweza kuifunga Nigeria na kuituma katika mashindano hayo kitu kinachoweza kuiduwaza dunia.

Comments
Post a Comment